Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

68 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

6. Mfungo binafsi . (Mt 14:23; Mk. 1:35). Kazi yetu ya kupambana na umaskini hutuweka katika jaribu la kupoteza ufahamu wetu wa mambo matakatifu. Tunaweza kusahau kwamba tunatumika ili kumpa Mungu heshima.

Ukurasa wa 48  8

a. Badala ya maisha ya shughuli nyingi na usumbufu, tunachukua muda kuelekeza maisha yetu katika utii kwa Mungu.

b. Dhamira ya Msingi : Tunadhamiria kuweka wakfu muda unaolingana na siku moja ya kazi (masaa nane) kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya maombi na tafakari ya maisha na kazi zetu. Wakati huu, tutajitenga na matumizi ya media.

c. Dhamira ya Juu : Tunadhamiria kuweka wakfu siku moja ya kazi (masaa nane) kila mwezi kwa ajili ya maombi na kutafakari juu ya maisha na kazi zetu. Wakati huu, tutajitenga na matumizi ya media.

7. Zaka . (1 Kor 16:2; 2 Kor 9:6-9). Kazi yetu ya kupambana na umaskini inaweza kusababisha dhana zisizo za kweli kuhusu pesa. Tunaweza pia kupoteza ukweli kwamba sababu kuu ya umaskini ni ukosefu wa haki za kiuchumi, jambo ambalo liko nje ya mamlaka na udhibiti wetu wa moja kwa moja.

Ukurasa wa 48  9

4

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

a. Badala ya kuhangaikia pesa, au kuabudu pesa, tunatoa kwa ukarimu.

b. Dhamira ya Msingi : Kujitolea kutoa angalau 1% ya mapato yetu yote kwa kanisa letu la mahali pamoja na mashirika yanayosaidia maskini kiuchumi.

c. Dhamira ya Juu : Kujitolea kutoa angalau 10% ya mapato yetu yote kwa kanisa letu la mahali pamoja na mashirika ambayo yanasaidia maskini kiuchumi.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker