Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
70 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Maswali yafuatayo yalikusudiwa kukusaidia kutafakari kuhusu maudhui yaliyomo katika Kanisa Lisilo la Kawaida , Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , na video ya Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini . Jibu kwa uwazi na kwa ufupi (tafakari maswali haya na uyajibu katika Jukwaa na uwe tayari kuyajadili katika mkutano wetu wa ana kwa ana). 1. Sura ya Kwanza ya kitabu cha Kanisa Lisilo la Kawaida inaitwa “Utetezi Pekee Hautoshi.” Je, mwandishi anajaribu kutuma ujumbe gani? 2. Je, utetezi/huduma yako imeathiri vipi utambulisho wako? 3. Ni kwa njia gani za kiutendaji umefungamanisha utetezi wako na imani yako? 4. Je, ni nidhamu ngapi kati ya nane zilizoelezewa hapo juu ambazo unaweza kuweka dhamira ya msingi kuzifanyia kazi? Ni nini kinakuzuia kuweka dhamira ya msingi kwa ajili ya nidhamu zote nane? 5. Je, ni nidhamu ngapi kati ya hizo nane ambazo unaweza kuwekea dhamira juu? Ni nini kinakuzuia kuweka dhamira ya juu kwa ajili ya zote nane? Somo hili linatoa theolojia ya vitendo kuhusu kutendea kazi Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini . • Kazi yetu ya utetezi dhidi ya umaskini inapaswa kujengwa juu ya msingi wa maisha yetu ya kiroho. • Mapokeo Makuu ya Kanisa yametoa njia zilizothibitishwa za kumweka Mungu kama kitovu cha maisha yetu. • Utetezi pekee hautoshi kubadilisha ulimwengu unaotuzunguka. • Kanisa lina jukumu muhimu katika kuboresha maisha ya wale walio katika hali ya umaskini na mitaa yao. • Kanisa lisilo la kawaida linawezesha, linashirikiana, na kuwafikia watu binafsi na taasisi zilizomo katika mitaa jirani.
Maswali na Majibu yaWanafunzi
Ukurasa wa 49 12
UHUSIANISHAJI
Muhtasari wa Dhana Kuu
4
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Sasa ni wakati wako wa kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu somo letu, Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini . Je, una maswali gani, ukizingatia mambo ambayo umejifunza hivi punde?
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker