Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 4 | MI ENENDO YA MA I SHA NA KAZ I YA KUPAMBANA NA UMASK I N I / 71

MFANOHALISI

Baada ya kukamilisha somo hili, rejea mfano halisi ulioelezwa hapo awali katika somo hili. Je, unaweza kutoa jibu gani la tofauti, kwa kuzingatia maudhui ya somo hili? Unafanya Kazi ya Kupambana na Umaskini katika mitaa ya jirani hapo mjini na unakutana na mwenzako kwenye duka lililopo kwenye kona. Anakuuliza kama una muda wa kutosha wa kuzungumza. Baada ya kutembea hadi ofisini kwake na kuanza kuzungumza, ni dhahiri kuwa ana hasira na ni mwenye kuchanganyikiwa. Amelemewa na changamoto anazokabiliana nazo kila siku. Changamoto hazikushtui kwa sababu hata wewe unakutana nazo. Hata hivyo, kinachokushtua ni sauti yake na kile anachosema. Anahisia za kibeuzi sana kwa habari ya watu wa mitaa hiyo na mashirika yaliyoanzishwa ili kuwasaidia, ikiwa ni pamoja na kanisa lake la mahali ambalo ameacha kuhudhuria. Malalamiko yake yanahusu kutothaminiwa kwa namna alivyojitoa na jinsi alivyochoka kimwili. Ungemwambia nini? Ili kuepuka mitego ya ubeuzi na uchovu sugu katika kazi ya kupambana na umaskini, ni lazima tutekeleze nidhamu za msingi za kiroho kama zinavyofundishwa katika Mapokeo Makuu ya Kanisa. Kujihusisha kwa uaminifu katika nidhamu hizi za kiroho kutafanyika kuwa hatua ya kukabiliana na kukusaidia kuepuka kutumbukia katika kazi hatarishi ya kupambana na umaskini na kutumika kama kichocheo cha kukuza imani yako na kudumisha afya yako ya kiroho huku ukisaidia wengine. Ikiwa una nia ya kufuatilia kwa kina baadhi ya mawazo kutoka kwa somo hili, Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: • Allsman, Don, and Don L. Davis. Piga Vita Vizuri vya Imani: Uwajibikaji wako katika mpango wa Mungu . Wichita: TUMI, 2014. • Davis, Don L. Mizizi Mitakatifu: Kidokezo cha Namna ya Kurejesha Mapokeo Makuu , Toleo la 2, Wichita: TUMI, 2010, 2017, 2024. • Carter, Ryan. Guard the Good Deposit: The Great Tradition for the Whole Church . Wichita: TUMI, 2019.

Ukurasa wa 50  13

Marudio ya Tasnifu ya Somo

4

Nyenzo na Bibliografia

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

Chukua muda kutafakari jinsi Roho Mtakatifu anavyoweka muunganiko kati ya maarifa ya somo hili la Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini na maisha na huduma yako. Je, unawezaje kufikiria, au kutenda tofauti katika hali halisi kulingana

Kuhusianisha Somo na Huduma

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker