Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
86 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Neno Linaloumba
Mch. Dkt. Don L. Davis
MAUDHUI
Neno la Mungu ni njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu anaumba maisha mapya ndani ya wale wanaoamini. Kwa hiyo, kupokea Neno na kudumu katika Neno hili la Mungu lililopandikizwa ndani yetu ni ishara ya kweli ya ufuasi na kufanywa wana wa kweli katika familia ya Mungu. Kama watakatifu wa Mungu, tunapokea Neno la Mungu pamoja katika jamii yake ya agano. Hatimaye, kwa sababu ya kutegemeka kwa Neno, ndilo pekee linaloweza kututangazia kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa, ambalo ni utukufu wa Mungu Mwenyezi. Lengo letu katika somo hili, Neno Linaloumba , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Neno la Mungu limebeba uzima wa Mungu mwenyewe, na kwa sababu hiyo, hakuna hali ya kiroho au dini ya kweli inayowezekana bila nguvu zinazotoa uhai za Neno la Mungu. Mungu huumba maisha mapya kwa waamini kupitia Neno lake, likiangaziwa na Roho Mtakatifu. • Ishara ya kweli ya ufuasi ni kukaa ndani na kuendelea katika upokeaji endelevu wa Neno la Mungu kama roho na kweli. Ukomavu wa kiroho unahusishwa moja kwa moja na kusikia na kutii Neno la Mungu katika Kanisa. • Kwa sababu ya mamlaka yake isiyoweza kukosea, ni Neno la Mungu pekee linaloweza kutupatia kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa, ambalo ni kumletea Mungu heshima na utukufu katika mambo yote.
Muhtasari
1
M A S O M O Y A B I B L I A
I. Neno la Mungu Limebeba Uzima wa Mungu Mwenyewe, na Kwa sababu hiyo Linaumba Maisha Mapya ndani yaWale Wanaoamini.
Muhtasari wa Video
A. Neno hujenga maisha ya kiroho kwa kuitikia imani katika kazi ya Yesu Kristo.
1. Neno la Mungu ni la msingi katika kuumba maisha mapya ya kiroho ndani ya mwamini.
a. Yakobo 1:18
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker