Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 1 | UONGOFU NA WI TO : NENO L I NALOUMBA / 89
b. Yos. 1:8
B. Ukuaji na ukomavu wa kiroho unategemea kujilisha kweli za Neno la Mungu linaloumba na kutoa uzima.
1. Waamini wanapaswa kutamani maziwa yasiyogoshiwa ya Neno la Mungu ili waweze kukua wanapojilisha, 1 Pet. 2:2.
2. Paulo, katika changamoto yake kwa wazee wa Efeso, aliwaweka katika mikono ya Mungu, na kwa Neno la neema yake “ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa,” Mdo 20:32.
1
3. Wakolosai wanahimizwa kuruhusu Neno la Mungu likae kwa wingi ndani yao, Kol. 3:16.
M A S O M O Y A B I B L I A
4. Paulo anampa Timotheo agizo lenye mamlaka la kujifunza ili kujionyesha kuwa mtenda kazi aliyekubaliwa na Mungu anapokuwa akilitumia (kuligawa) Neno la kweli kwa usahihi, 2 Tim. 2:15.
5. Kuna njia nyingi za kudumu katika Neno la Mungu.
a. Tunapaswa kulisoma . Ufunuo 1:3 inaahidi baraka kwa wale wanaosoma Neno la Mungu.
b. Tunapaswa kulikariri . Katika Zaburi 119:11 Daudi anasema anaficha Neno la Mungu moyoni mwake ili asije akamtenda Bwana dhambi.
c. Tunapaswa kulitafakari . Zaburi 1:3 inasema kwamba mcha Mungu hutafakari na kutafuna Neno la Mungu mchana na usiku.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker