Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
90 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
d. Tunapaswa kulisoma . Waberoya wanaitwa “watu waungwana zaidi” kuliko Wathesalonike katika Matendo 17:11 kwa sababu hawakusikia tu maneno ya Mtume Paulo, bali walisoma Maandiko kila siku ili kuthibitisha Injili ya Paulo. e. Tunapaswa kulisikia likihubiriwa na kufundishwa katika Kanisa. Hatupaswi kudharau unabii, bali lisikie Neno kwa maana, kama Warumi 10:17 inavyodokeza, “imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa Neno la Kristo.”
f. Tunapaswa kulijumuisha katika maisha na mazungumzo yetu yote . Neno linaloumba lazima liwe nguvu inayotawala maishani mwetu kama inavyosemwa katika maneno ya Shema, Kum. 6:4-9.
1
M A S O M O Y A B I B L I A
C. Neno hili la uumbaji la Mungu lazima lisikike na kupewa utii katika mazingira ya jumuiya ya Kikristo.
1. Msidharau unabii, wala msimzimishe Roho Mtakatifu; 1 Thes. 5:19-22.
2. Neno litakuja katikati ya kusanyiko, 1 Kor. 14:26.
3. Mungu amelipatia Kanisa wanaume na wanawake waliopewa vipawa maalum na Roho Mtakatifu ili kufundisha Neno la Mungu, Efe. 4:11-13.
III. Neno Hufunua Kusudi la Milele la Mungu kwa Ulimwengu: Ili Vitu Vyote Vipate Kumpa Utukufu na Heshima kama Bwana.
A. Mshindo mmoja wa msingi wa nishati hupiga kutoka kwenye moyo wa Hadithi ya Kiungu. Vitu vyote viliumbwa ili kuleta utukufu, heshima, na sifa kwa Bwana na Jina lake tukufu.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker