Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | UONGOFU NA WI TO : NENO L I NALOUMBA / 91

1. Vitu vyote viliumbwa kwa kusudi la Mungu lililokusudiwa, Mit. 16:4.

2. Vitu vyote mbinguni na duniani, vinavyoonekana na visivyoonekana, malaika wote, viumbe vyote, wanadamu na wanyama, na vyote vilivyoko viliumbwa na Mungu na kwa utukufu wake.

a. Kol. 1:16

b. Ufu. 4:11

1

c. Zab. 150:6

3. Taifa la Israeli, watu waliochaguliwa na Mungu, walichaguliwa kwa ajili ya utukufu wake mkuu.

M A S O M O Y A B I B L I A

a. Isa. 43:7

b. Isa. 43:21

c. Ona Isa. 43:25; 60:1, 3, 21

4. Mungu huwaokoa wanadamu ili kujiletea utukufu na heshima, Rum. 9:23; Efe. 2:7.

5. Huduma zote na kazi ambazo watu wa Mungu hutimiza mwisho wa yote zinapaswa kufanywa kwa utukufu wa Mungu, 1 Kor. 10:31; Yoh. 15:8; Mt. 5:16.

6. Kusudi kuu la mwamini: ushuhuda binafsi kwa utukufu wa Mungu katika Kristo, na kushiriki katika utukufu huo wakati wa kufunuliwa kwake.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker