Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

92 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

a. Yoh. 17:22

Ikichukuliwa katika ujumla wake, Biblia inatofautiana katika ujumbe na kusudi lake na kitabu kingine chochote ulimwenguni. Inasimama juu kabisa katika kuakisi kwake nafasi ya [binadamu] na fursa [yake] ya wokovu, tabia kuu na kazi ya Yesu Kristo kama Mwokozi wa pekee, na inatoa kwa undani utukufu usio na kikomo ambao ni wa Mungu mwenyewe. kiumbe na kufunua mpango ambao kwa huo [wanadamu] wote katika kutokamilika [kwao] wote wanaweza kupatanishwa katika ushirika wa milele na Mungu wa milele. ~ Lewis Sperry Chafer. Major Bible Themes . Grand Rapids: Zondervan, 1974. uk. 29. Ni kitabu kimoja kinachomfunua Muumba kwa

b. Kol. 3:4

B. Tunapojinyenyekeza chini ya Neno la Mungu linaloumba, tunapata nguvu na mwelekeo ili kutimiza kusudi hili la kumheshimu na kumtukuza.

1. Linafunua nia na matamanio yetu ya ndani, Ebr. 4:12.

2. Linaiweka mioyo yetu inayoyumba-yumba katika mstari sanjari na ukuu wa kusudi la milele la Mungu.

1

M A S O M O Y A B I B L I A

a. Maandiko kama furaha na shangwe ya mioyo yetu, Yer. 15:16.

b. Neno la Mungu huleta mguso mkubwa ndani kabisa ya mioyo yetu tunapojisalimisha chini ya nguvu zake, Yer. 20:9.

3. Linatugeuza kwa kufanya upya nia zetu kuyaelekea mapenzi kamili ya Mungu, Rum. 12:1-2.

Hitimisho • Neno la Mungu limebeba uzima wa Mungu mwenyewe na ni njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu anaumba maisha mapya ndani ya wale wanaoamini. • Wanafunzi wa kweli wa Yesu Kristo hukaa katika Neno hili lililopandikizwa ndani yao. • Roho Mtakatifu anatufundisha kwamba kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa ni kumtukuza Mungu Mwenyezi. • Maandiko, Neno linaloumba, hutuwezesha kumtukuza Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu tunapoishi chini ya utawala wa Mungu.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker