Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 1 | UONGOFU NA WI TO : NENO L I NALOUMBA / 93

Maswali yafuatayo yalikusudiwa kukusaidia kufanya mapitio ya maudhui yaliyomo katika video ambayo ililenga sifa za uzima wa Neno la Mungu maishani mwetu. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, jenga hoja zako kwa kutumia Maandiko! 1. Je, Biblia inaelezaje jukumu ambalo Maandiko hutimiza katika kutoa maisha mapya kwa yule anayemwamini Kristo? Je, imani ina jukumu gani pamoja na Neno ili kuumba kuzaliwa upya? 2. Ni kwa njia gani jaribu la Yesu linatufundisha kuhusu nguvu ya Neno la Mungu juu ya maisha yetu? Yesu alitaja kweli gani alipokabiliana na shetani na madanganyo yake nyikani? 3. Roho Mtakatifu ana jukumu gani katika kumsaidia mtu wa kiroho aelewe maana ya Maandiko Matakatifu? Vipi kuhusu mtu wa asili – anaweza kuyaelewa? Ikiwa jibu ni ndiyo, kwa nini; ikiwa jibu ni hapana, kwa nini? 4. Ishara ya kweli ya ufuasi katika Yesu Kristo ni ipi? Eleza uhusiano uliopo kati ya kukua kiroho na kujilisha Neno la Mungu. 5. Ni zipi baadhi ya njia ambazo Maandiko yanafundisha ambazo mtu anaweza kudumu katika Neno la Mungu? Je, kudumu katika Neno kuna uhusiano gani na kuishi katika jumuiya ya Kikristo? 6. Ni watu gani hasa ambao Mungu amelipatia Kanisa ili kulisaidia kuelewa na kutumia Neno la Mungu? Jukumu lao ni lipi katika kusaidia kuwakamilisha Wakristo kwa ajili ya kazi ya huduma? 7. Kulingana na Maandiko, kusudi la milele la Mungu kwa ulimwengu ulioumbwa ni lipi? 8. Hatimaye, ni kusudi gani kuu ambalo Mungu ameweka kwa waamini, na ni kwa jinsi gani wanapaswa kutimiza kusudi hilo maishani mwao? 9. Ni kwa njia gani Maandiko (Biblia) ni ya pekee na yanapita vitabu vingine vyote ulimwenguni? 10. Tunaweza kutazamia nini kutokea katika mioyo yetu na maishani mwetu tunapojitiisha chini ya Neno la Mungu linaloumba? Elezea.

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu Ukurasa wa 70  6

1

M A S O M O Y A B I B L I A

UHUSIANISHAJI

Somo hili linaangazia baadhi ya vipengele muhimu vya uwezo wa uumbaji wa Neno la Mungu, kwa ujumla katika uumbaji wa ulimwengu, na kimahususi, katika uumbaji wa maisha mapya ya

Muhtasari wa Dhana Muhimu Ukurasa wa 71  7

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker