Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
94 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
kiroho ndani ya moyo wa mwamini. Kwa kila maana, elimu ya Neno la Mungu ni muhimu katika kuelewa kazi ya Mungu ulimwenguni, na katika historia yote ya mwanadamu. • Maandiko Matakatifu ni Neno la Mungu lililo hai na la milele. Linahusishwa moja kwa moja na nafsi ya Mungu na kazi yake. • Neno la Mungu, likiwa limeletwa na Roho Mtakatifu na hivyo kubeba uzima wa Mungu mwenyewe, ni chombo muhimu ambacho kupitia hicho maisha mapya yanaumbwa kwa wale wanaomwamini Yesu. Ujumbe wa Injili ni mbegu ya kiroho inayotufanya tuzaliwe kutoka juu. • Ishara halisi ya ufuasi wa kweli katika Kristo ni kukaa na kuendelea katika Neno la Yesu, ambalo huwaweka huru waamini. • Mungu amempa kila mwamini Roho Mtakatifu ili tuweze kuelewa na kufahamu maana ya Maandiko ambayo aliyavuvia (1Kor. 2:9-16 linganisha na 2 Pet. 1:21-22). • Roho Mtakatifu anatufundisha kwamba kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa ni kumtukuza Mungu Mwenyezi (Isa. 43:7; Mit. 16:4; 1 Kor. 10:31). • Maandiko, Neno linaloumba, hutuwezesha kumtukuza Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu tunapoishi chini ya utawala wa Mungu. Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu nguvu ya Neno linaloumba. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia maarifa ambayo umejifunza hivi punde? Pengine maswali yaliyo hapa chini yanaweza kuibua mjadala wenu pamoja, na kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. • Tunaposema kwamba Maandiko yamevuviwa na Mungu, je, tunamaanisha “hati asilia” (yaani, hati ambazo manabii na Mitume waliandika), tafsiri, nakala za tafsiri, au kila kitu? • Imani yetu ya kwamba Mungu aliumba ulimwengu kupitia Neno lake ina matokeo gani kuhusiana na mjadala juu ya nadharia ya mageuzi ( evolution )? Je, nadharia ya mageuzi ni jambo tunalohitaji kuhangaikia au la? • Ikiwa Neno la Mungu li hai na lina nguvu na uwezo wa kuumba, kwa nini halionekani kufanya kazi namna hiyo katika moyo wa kila mtu anayelisikia? Kwa nini watu wengi sana wanaukataa ujumbe wa Neno leo?
1
M A S O M O Y A B I B L I A
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
Ukurasa wa 71 8
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker