Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 4 1

• Tunapoangalia hali – maisha ya watu na mitaa – daima tuna imani kwamba Mungu anaweza kushinda hili na kwamba anaweza kututumia kuleta mabadiliko katika hali hiyo.

Jukumu letu kamaWafanyakazi wa Kiukombozi dhidi ya Umaskini Umaskini ni hali, sio utambulisho. 1. Kosa kubwa la jamii ni kwamba tabaka letu katika jamii linakuwa utambulisho wetu. Hili lina athari kubwa kwetu. 2. Tunapaswa kulishughulikia hilo, na tusiruhusu hali yetu ya kijamii kufanyika utambulisho wetu WOTE. 3. Hasa kwa wale walio katika umaskini, uwepo na utu wao, kwa mujibu wa mtazamo wa kijamii, unawekwa kwenye ngazi ya chini ya ubinadamu kwa sababu hawana rasilimali nyingi za kifedha. Wengi hawataki kuishi katika mitaa yao. 4. Mungu huwatumia watu kwamba ni matajiri, au hawana pesa kabisa, au wako mahali fulani katikati. 5. Na kama dokezo la ziada – utambulisho wa rangi umeunganishwa katika haya yote pia. Huenda usijue ubaguzi wa rangi unaanzia wapi, na matabaka ya kijamii yanaishia wapi. Vyote vimefungwa pamoja kwenye duara moja kubwa, kiasi ambacho ikiwa wewe ni mweusi au maji ya kunde, inachukuliwa kuwa wewe ni maskini au unaishi katika umaskini au unajua kuhusu umaskini. 6. Mtazamo bora ni kuwaona watu walio katika umaskini kwa njia ile ile ambayo tungemwona mtu mwingine yeyote na sio kuwatafsiri kwa namna hasi. Mungu amewapa karama na talanta sawa sawa na zile ambazo amempa kila mtu. Ufalme wa Mungu unatembea kati yao kupitia nguvu za kanisa la mahali pamoja. 7. Katika Waefeso, Mtume Paulo alielewa kwamba utambulisho wake haukuwa kwenye hali yoyote ile aliyojikuta nayo, bali utambulisho wake daima ulikuwa katika ukweli kwamba alikuwa mtoto wa Mungu na mfuasi wa Yesu Kristo.

 4 Ukurasa wa 56 Muhtasari wa Kipengele cha III

3

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online