Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
4 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
8. Kwa sababu Kristo yu pamoja nasi, hivyo ndivyo tunavyoweka imani, tumaini na tegemeo letu ndani yake. Tembea kwa imani huku ukipanga upya nguvu za kimfumo za binadamu. 1. Utetezi wetu na kuingia katika shughuli za kupigania haki za kijamii ni katika jicho la Mungu. Tunataka Mungu atembee katika hali hizi. 2. Tunachochewa na kanuni za kitheolojia. Kanuni za kijamii na kitamaduni huboresha kanuni hizo za kitheolojia. Unaweza kuambatanisha uwanda wa kijamii na kitamaduni baada ya msingi wa kitheolojia kuwa umewekwa. 3. Tunapokabiliana na nguvu hizo ambazo zinajaribu kuwafanya watu kuwa chini ya hadhi ya ubinadamu na kujaribu kufanya jamii kuwa chini ya kile ambacho ina uwezo wa kufanya... tunajua kwamba tunachofanya ni kwa imani katika Mungu. Bila kujali matokeo, haibadilishi ukweli kwamba kile tunachojitahidi kutekeleza ni kuufanya ulimwengu huu kuwa mahali bora zaidi. Sasa waruhusu wanafunzi watoe maoni yao juu ya kile kilichowasilishwa. Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya mada ambazo zinaweza kujadiliwa ikiwa unahitaji kuendeleza mjadala. (KUMBUKA: Haulazimiki kuzitumia. Ikiwa darasa lako linakwenda vizuri, waruhusu wanafunzi wajadili kwa uhuru). • Kanisa linahitaji kufafanua uhusika wake katika mageuzi na mabadiliko ya kijamii. Linapokuja kwenye masuala ya kijamii yanayotokea duniani kote, mara nyingi, Kanisa liko kimya sana. Halitaki kujihusisha na masuala ya kisiasa au huamini kuwa haya ni mambo ya kisiasa na hayapaswi kuhusishwa na Kanisa. • Kwa sababu makanisa yako kimya, vijana wengi wanatafuta mahali na majukwaa ambapo wanaweza kupata utetezi.
3
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
5 Ukurasa wa 57 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online