Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 4 3

• Je, inawezekana kwa kanisa kufanya kazi pamoja na shirika lisilo la kimaadili au lenye kunyonya watu ikiwa ni kwa manufaa ya wote? • Ongoza kwa misingi ya Neno na kisha useme ukweli kuhusu hali za kijamii zilizopo. • Katika ngazi ya taasisi, kabiliana na udhalimu. Katika ngazi binafsi, Biblia inatuambia tutengeneze fursa kwa watu walio katika hali ya umaskini kuishi maisha yenye heshima ya utu zaidi na kubadili matabaka ya kijamii. Lakini wengine/wengi hawawezi kubadili matabaka ya kijamii. Ni muhimu kujua kwamba Yesu yuko pamoja nasi hata katikati ya mateso yetu. • Au tumia maswali ya majadiliano yafuatayo: 1. Je, ukombozi umebadilishaje maisha yako binafsi? 2. Dhana ya Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini inaleta tafsiri yayote kwako? Eleza kwa nini au kwa nini sivyo. 3. Je! ni tofauti gani kuu kati ya Kazi ya Kupambana na Umaskini kwa misingi ya kimaadili na ile ya kiukombozi ? Jadili Mfano Halisi: Umekuwa ukifanya kazi na Sheri kwa miaka mitano. Kwa maelezo yote, Sheri ni mwanamke mzuri na mwenye imani thabiti. Yeye huhudhuria kanisani kila Jumapili ambayo hajapangiwa kufanya kazi katika hoteli kama mhudumu. Mara zote huleta nyumbani pesa za kutosha kujikimu yeye na watoto wake watatu, kwa kuwa baba yao hachangii sana. Hivi sasa, amekasirika kwa sababu amegundua kwamba mmoja wa wanawe amefukuzwa kutoka kwenye shule binafsi ya Kikristo ambayo wewe ulichangia sana kuandikishwa kwake hapo. Kwa upande mmoja, anahisi kuaibishwa; kwa upande mwingine, anahisi ni kama haonekani mbele za Mungu kwa sababu, kwa maoni yake, shule imeyafanya hayo kwa sababu za ubaguzi wa rangi na tabaka la kijamii analotokea. Unadhani utamweleza nini Sheri?

3

K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I

 6 Ukurasa wa 57 Mfano Halisi

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online