Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
4 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Waache wanafunzi wajibu hili, lakini hapa kuna mapendekezo ya baadhi ya vipengele vya kuanza navyo: • Kwa vile nilishiriki katika kumwandikisha kijana huyo shuleni hapo, ningechukua jukumu la kuzungumza na uongozi ili nisikie upande wao kisha nisikie kutoka kwa kijana huyo. • Kwa kuwa inasemekana katika mfano kwamba baba hana mchango mkubwa sana katika maisha ya watoto, ningeona ikiwa kuna mwanamume kanisani ambaye anaweza kuwa mshauri wake. Angeweza kutumia mwongozo thabiti wa kibiblia kwa mwanaume. • Mwishoni mwa mazungumzo, eleza sababu ya kufukuzwa na uone ikiwa hilo linabadilisha maoni ya mtu yeyote: Kijana huyo alivaa fulana moja ya kaka yake mkubwa iliyokuwa na jani la bangi. Kutokana na utamaduni alimokulia, hilo halikuwa tatizo. Hakuwa anatumia au kuuza madawa ya kulevya. Shule ilihisi kuwa ni kosa na badala ya kuzungumza ili kuona nini kinaweza kuwa funzo kutoka kwa mtazamo wa kiutamaduni wa pande zote mbili, walisema kwamba hawaweze kutetea dawa za kulevya na kuitangaza tabia yake kuwa dhambi na mbaya na kumfukuza. Shule inaua nzi kwa kutumia nyundo.
3
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online