Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 4 5
Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini
SOMO LA 4
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini , Somo la 4: Mienendo ya Maisha na Kazi ya Kupambana na Umaskini . Somo hili linaelezea matendo ya kiroho kuhusiana na Kazi ya Kupambana na Umaskini, ambayo yanahusiana maja kwa moja na Mapokeo Makuu ya Kanisa. Ni muhimu uwasaidie wanafunzi wako kuelewa maana ya Mapokeo Makuu . Ufuatao ni ufafanuzi mzuri: “Mapokeo Makuu yanawakilisha kiini kikuu cha misingi ya imani na desturi za Kikristo zinazotokana na Maandiko ambazo zilitawala kati ya wakati wa Kristo na katikati ya karne ya tano” (Dkt. Don Davis, Sacred Roots, TUMI: 2010, uk. 74). Huu hapa ni upanuzi muhimu wa ufafanuzi huu: “Ni urithi wa namna Wakristo wa mwanzoni walivyoshughulika na Maandiko ambayo kimsingi yaliliumba na kuliweka kanisa kwenye sura nzuri ambayo tumeifahamu. Kanisa la kwanza lilijenga kanuni ya imani (ukiri) inayotoa muhtasari wa kiini cha imani kutoka katika Maandiko. Waliunda huduma ya Neno na Meza (Ushirika Mtakatifu) ambayo iliongoza kila kusanyiko la ibada kwenye Injili ya Kristo na Ufalme wake. Waliifanya kalenda ya sikukuu za Kiyahudi kuwa ya Kikristo ili kuyafanya maisha yao ya kiroho yaendane na hadithi ya Mungu katika Kristo. Neno la Mungu lilikaa kwa wingi ndani yao na wakawa nuru inayomwakilisha Kristo na Ufalme wake ulimwenguni. Imani na desturi zao zikawa Mizizi Mitakatifu ya kila tawi la kanisa” (Ryan Carter, Guard the Good Deposit , TUMI: 2019, uk. 11-12). Kazi ya Kupambana na Umaskini imekuwa muhimu kwa Kanisa tangu siku zake za awali. Mapokeo Makuu yalizaliwa si mbali na umaskini bali katikati yake. Kimsingi, Wakristo wengi wa Kanisa la Kwanza walitoka katika jamii za watu maskini, wa hali ya chini, na waliodharauliwa. Msimamo hasa wa somo hili ni kwamba Kazi ya Kiukombozi dhidi ya Umaskini haiwezi kutenganishwa na imani na desturi za Mapokeo Makuu. Ni muhimu sana uwasaidie wanafunzi wako kudumisha muunganiko sahihi katika fahamu zao kati ya utambulisho wetu sisi kama Kanisa na kile tunachofanya ulimwenguni. Ikiwa kwa kweli tunatumai kuona watu na mitaa ikikombolewa, lazima chimbuko na nguzo ya kazi yetu viwe ni maisha thabiti ya kanisa yenye mizizi katika Mapokeo Makuu.
1 Ukurasa wa 61 Utangulizi wa Somo
4
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online