Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
4 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Nidhamu za kiroho zilizoainishwa katika somo hili zimekusudiwa kukusaidia wewe na wanafunzi wako kukumbatia na kuakisi imani hii. Ni njia za vitendo za kutusaidia kuyaishi maisha yetu ya pamoja, safari ya pamoja, nidhamu ya pamoja na maungamo ya pamoja.
Katika kufanya kazi kwenye jamii zenye umaskini na kuwahudumia wale ambao maisha yao yanalemewa na mateso ya kiroho, kimwili, au kisaikolojia, itakuwa changamoto kudumisha ari na nguvu unayohitaji. Unaweza kupata ari hiyo na nguvu kutoka katika Mienendo hii ya Maisha. Hii inaweza kutulinda dhidi ya uchovu, kuwa sumu sisi wenyewe, na dhidi ya msongo wa mawazo uliopitiliza. Miezi mitatu tu ya kuishi na kufanya kazi katika jamii ambazo zimefadhaika na kuharibikiwa kiuchumi na zilizo chini ya shinikizo kubwa kijamii, inatosha kabisa kuharibu kujitoa kwako kote ulikoanza nako. Watu walioitwa kuhudumu katika jamii hizi mara nyingi hufikiri kwamba kwa sababu Mungu amewaita katika Kazi ya Kupambana na Umaskini, watakuwa sawa. Wanachogundua baadaye ni kwamba maisha yao binafsi, akili zao, miili yao, ukosefu wa usingizi, saa nyingi za kazi, mambo yote yanayoambatana na kuhudumu katika jamii hizi huathirika. Wanagundua kuwa wao wenyewe ndio walengwa na wahanga wa shambulio la shetani. Huwezi kuwapa wengine kile ambacho wewe mwenyewe huna. “Huwezi kutoa kile ambacho huna, na huwezi kupoteza kile ambacho hujawahi kuwa nacho” (Muddy Waters). Kwa hivyo jambo la kwanza juu ya yote katika kufanya huduma kwenye mitaa iliyo hatarini ni utunzaji wa nafsi yako.
2 Ukurasa wa 63 Muhtasari
4
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
Uanachama wa Kanisa • Jitolee kuwa mshirika hai ndani ya kanisa la mahali pamoja lenye afya kwa madhumuni ya ushirika, mafundisho, maombi, huduma, na maendeleo binafsi.
3 Ukurasa wa 65 Muhtasari wa Kipengele B, 1
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online