Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
5 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
• Kundi la wachungaji fulani waliohusika na masuala ya jamii katika makanisa yao lilishauriwa kwamba waweke mabango kwenye milangoni yao yenye maneno: “Hatufanyi kazi siku ya Jumatatu.” Hii ni kwa sababu kila siku na kila saa kulikuwa kuna mtu anayehitaji kuwauliza au kuwaomba jambo fulani. Wao walifikiri wazo hilo lilikuwa la kishetani na kinyume na kielelezo cha Yesu. Kwa kweli unaweza kuwafundisha kwa mifano kuhusu mipaka yako ni ipi, yumkini hatimaye wanaweza kujifunza kuwa na mipaka pia. • Baada ya kutumika kwa miaka kumi na minne kama wamishenari mahali ambapo kila mara watu walikuwa wakiomba na kuuliza kitu (kila saa, mamia ya watu wakihudumiwa na watu wawili), mmoja wa wamishenari hao wawili alikuwa na dalili ambazo ziligunduliwa kuwa ni mfadhaiko na msongo wa mawazo. Waligundua kuwa likizo na mapumziko ni ya muhimu sana. • Au tumia maswali ya majadiliano yafuatayo: 1. Kwa nini ni muhimu kwamba shughuli za utetezi zifanyike katika misingi na nidhamu za kiroho? 2. Ni kwa njia zipi za vitendo umeungamanisha kazi yako ya utetezi na imani yako? 3. Je, ni nidhamu ngapi za kiroho unazojihusisha nazo mara kwa mara? Jadili Mfano Halisi: Unafanya Kazi ya Kupambana na Umaskini katika mitaa ya jirani hapo mjini na unakutana na mwenzako kwenye duka lililopo kwenye kona. Anakuuliza kama una muda wa kutosha wa kuzungumza. Baada ya kutembea hadi ofisini kwake na kuanza kuzungumza, ni dhahiri kuwa ana hasira na ni mwenye kuchanganyikiwa. Amelemewa na changamoto anazokabiliana nazo kila siku. Changamoto hazikushtui kwa sababu hata wewe unakutana nazo. Hata hivyo, kinachokushtua ni sauti yake na kile
4
K A Z I Y A K I U K O M B O Z I D H I D I Y A U M A S K I N I
13 Ukurasa wa 71 Mfano Halisi
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online