Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

1 3 0 /

M U N G U B A B A

Sasa, chukua muda kujadili na wenzako baadhi ya maswali ya ufafanuzi kuhusu mawazo na dhana ambazo ziliibuka kupitia video. Katika namna fulani, ufahamu wa kutosha wa kile ambacho Maandiko yanafundisha kuhusu wema wa Mungu Baba Mwenyezi ni muhimu kabisa kwa mtu ambaye anahitaji kuwapa wengine maelezo yaliyowazi na ya kushawishi kumhusu Bwana. Wema wa Bwana unatumika kama msingi wa wokovu wetu, toba yetu, na hata wa mahusiano yetu na Mungu kupitia Yesu Kristo, ambaye neema yake ilituongoza kwa Mungu. Kwa hiyo, hakikisha unauelewa wema wa Mungu na sifa zote zinazouzunguka. Majibu yako yawe ya wazi na mafupi, na inapowezekana uyaunge mkono kwa Maandiko! 1. Kuna uhusiano gani kati ya wema wa ajabu wa Mungu na tabia yake ya kiadili? Inamaanisha nini tukisema kwamba “Mungu huonyesha ukamilifu wake wa kiadili kupitia sifa za usafi, uadilifu, ukamilifu, na upendo usio na mipaka?” 2. Nini maana ya utakatifu wa Mungu? Kuna uhusiano gani kati ya haki na utakatifu wa Mungu? Ni kwa njia gani Mungu huonyesha usafi wake kamili wa kiadili kupitia hukumu zake za haki ulimwenguni? 3. Kama kielelezo cha uadilifu na ukamilifu wake, inamaanisha nini kusema kwamba Mungu Baba Mwenyezi ni halisi? Ni mambo gani yanayojumuishwa katika msistizo kwamba Baba ni wa kweli? Ni vipengele gani vinahusishwa katika msistizo kwamba Baba ni mwaminifu? 4. Upendo wa Mungu unahusisha ukarimu wake; nini hasa maana ya hilo? Elezea maana ya neema ya Mungu. Ni kwa namna gani neema ya Mungu inahusiana na rehema zake? Ni kwa namna gani uvumilivu wa Mungu unatuonyesha wema wake sisi na uumbaji wake? 5. Katika kutafuta kuzielewa sifa za wema wa Mungu, je kuna njia ya kuziona pamoja, kwa ujumla, “kuziweka pamoja” tunapozitafakari? Elezea jibu lako. 6. Ni kwa jinsi gani uelewa kamili wa kibiblia wa wema wa Mungu unaweza kuathiri maisha yetu na huduma zetu binafsi? Kwa maoni yako, ni namna ipi ungedhani kuwa ni bora ya kuwashirikisha wengine kuhusu wema wa Mungu? Elezea jibu lako.

Sehemu ya 1

Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu page 298  4

4

Made with FlippingBook - Share PDF online