Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 1 3 1
M U N G U B A B A
Mungu kama Baba: Wema wa Mungu Sehemu ya 2: Sifa za Kiadili za Ukali
Mch. Dkt. Don L. Davis
Ufahamu wa ghadhabu ya Mungu, sifa ya kimaadili ambayo kwa kawaida inahusishwa na ukali wa Mungu na si wema wake, ni muhimu kabisa kwa yeyote anayedai kuwasilisha picha kamili ya Biblia ya Mungu Baba Mwenyezi. Kama fundisho kuu la Maandiko, ni lazima tujitahidi kuelewa ghadhabu ya Mungu katika muunganiko na wema wake, jambo linaloweza tu kutimizwa kwa uchunguzi wa karibu wa uhusiano kati ya wema wa Mungu na ukali wake. Ingawa tunaweza kupata shida kuuelewa uhusiano huo, haujawahi na hautatokea kuleta mkanganyiko au mgogoro wowote ndani ya Mungu. Yeye ni Mungu mmoja wa kweli na atadumu hivyo milele, daima akitenda kwa upendo na haki kila mahali, katika neema na kweli. Lengo letu katika sehemu hii, Sifa za Kiadili za Ukali, ni kukuwezesha kuona kwamba: • Ghadhabu ya Mungu Baba Mwenyezi ni moja ya mafundisho makuu ya Maandiko Matakatifu, na kipengele muhimu cha ufunuo wa Mungu kwetu kuhusiana na nafsi yake. • Ghadhabu yaMungu, kama sifa ya kiadili ambayo kwa kawaida inahusishwa na ukali na si wema wa Mungu, lazima ichunguzwe kwa kuhusianishwa na wema wa Mungu. Upendo na haki lazima vieleweke kwa pamoja. • Mkanganyiko wowote tunaoweza kuuona kati ya utakatifu wa Mungu na upendo wake kiuhalisia si mkanganyiko wa kweli lakini ni ugumu tu wa fahamu zetu katika kuelewa kikamilifu sifa kamilifu za Mungu na asili yake ya pekee kama Mungu. • Katika ufahamu na tabia ya Mungu menyewe, hakujawahi kuwa na wala hakutakuwa na mkanganyiko wala mgogoro kati yake au kati ya sifa zake mwenyewe. • Kila mahali Mungu anapotenda na kufanya kazi, yeye ni Mungu mmoja wa kweli na atadumu milele katika sifa hiyo, daima akitenda kila mahali kwa upatanifu kamili wa upendo na haki yake, neema na kweli yake.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
4
Made with FlippingBook - Share PDF online