Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

1 3 2 /

M U N G U B A B A

I. Ghadhabu ya Mungu Baba Mwenyezi

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

A. Ufafanuzi (J. I. Packer, ghadhabu ya Mungu inarejelea hatua ya “Mungu kuingia katika tendo la kulipiza kisasi, kwa namna yoyote, dhidi ya wale waliomkaidi,” Knowing God, uk. 149).

Ikiwa tunataka kumjua Mungu, ni muhimu sana tukabaliane na ukweli kuhusu ghadhabu yake, haijalishi kwamba ukweli huo utaonekana wa kizamani kiasi gani, na pasipo kujali ni kwa kiasi gani tunauchukia ukweli huo. Vinginevyo, hatutaielewa Injili ya wokovu katika msingi wa ghadhabu ya Mungu, wala kazi ya upatanisho wa msalaba, wala ajabu za pendo la ukombozi wa Mungu. ~ J. I. Packer. Knowing God. Downers Grove: InterVarsity Press, 1993. uk. 156.

1. “Mungu kuingia katika… ”: ghadhabu ya Mungu ni kielelezo cha asili kamili ya Mungu (yaani, Biblia ina kiasi sawa cha rejea juu ya mada ya hasira, ghadhabu, na upendo wake).

2. “ ... tendo la kulipiza kisasi. . .”: ghadhabu ya Mungu inaonyeshwa katika matendo ya kulipiza kisasi, kama mwitikio wake dhidi ya wale waliokataa wito wake wa toba na/au badiliko.

3. “ ... kwa namna yoyote ...”: ghadhabu yaMungu inaweza kudhihirishwa kwa mafuriko au moto; ni mamlaka na ukuu wake pekee ndio huamua namna.

4

4. “ ... dhidi ya wale waliomkaidi”: ghadhabu ya Mungu (kama ilivyo kwa upendo wa Mungu) inaelekezwa kwa wale wastahilio kuipokea kwa namna anayochagua yeye.

B. Vipengele vya ghadhabu ya Mungu

1. Vipengele hasi: Yale ambayo si ghadhabu ya Mungu

a. Haifanyiki katika hali ya kigeugeu (mihemko, maamuzi ya ghafla, mwitikio wa bila kufikiri).

b. Kamwe haitolewi bila sababu (kwa upumbavu au isivyo haki).

Made with FlippingBook - Share PDF online