Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

9 0 /

M U N G U B A B A

3. Thibitisha usawa wa washiriki (katika utukufu, kiini, na ukuu).

Hitimisho

» Neno la Mungu linafundisha kwamba kuna Mungu mmoja tu, na bado Mungu huyu anajifunua kwetu kama Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. » Zaidi ya hayo, Maandiko hayafundishi tu kwamba Mungu ni Mungu mmoja, bali pia yanamzungumzia Mungu katika nafsi tatu – Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yameibuka kutokana na video. Fundisho la Biblia juu ya Utatu si rahisi wala jepesi kuelewa. Kinachopaswa kueleweka, hata hivyo, ni kwamba Utatu ni jaribio la kukubali kwa mamlaka na uaminifu wote ushuhuda wa kimaandiko kuhusu umoja wa Mungu kama Mungu mmoja, na wakati huo pia kukubali uungu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Fanyia mazoezi dhana kuu kuhusu fundisho hili muhimu, na uhakikishe kwamba unaouwezo wa kutetea madai yoyote unayotoa kwa kutumia Maandiko yenyewe (Mdo 17:11). 1. Nini maana ya “fundisho la Utatu ”? Neno hili linarejelea fundsho lipi laBiblia? 2. Fanya muhtasari juu ya namna Maandiko yanavyosisitiza kwamba Mungu ni mmoja, wakati huohuo, yakiuthibitisha uungu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. 3. Toa mifano ya baadhi ya uthibitisho wa kibiblia unaodai kwamba kila mshiriki wa Utatu (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) ni Mungu, (yaani, onyesha kutoka katika Biblia jinsi kila mshiriki wa Utatu alivyo na sifa za Mungu, anavofanya kazi ya Mungu, anavyoitwa Mungu,na kutumia mamlaka kama Mungu). 4. Ni kwa namna gani tunaweza kuthibitisha umoja wa Mungu, na wingi wa Mungu? 5. Nini maana na uhusiano wa nafsi za Mungu na kiini kimoja cha Mungu? Kanisa limejaribu kwa namna gani kuelewa mafundisho ya Biblia kuhusu Utatu? (toa mfano).

Sehemu ya 1

Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu

3

page 291  4

Made with FlippingBook - Share PDF online