Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 9 1

M U N G U B A B A

6. Kwa nini ni lazima kabisa kutosema kamwe kuwa wazo la Utatu linamaanisha miungu watatu? Kwa nini kanisa limekuwa makini sana kutofautisha Uungu mmoja wa Mungu huku likithibitisha nafsi tatu za Mungu? 7. Kanuni za Imani hutusaidiaje kuelewa jinsi jambo fulani lisivyo la kweli kuhusu Utatu? Je, Unaweza kukataa wazo lolote kati ya haya – umoja wa Mungu, utofauti kati ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, na usawa wa washiriki wote wa Utatu – na bado ukawa na mtazamo wa Utatu unaokubalika?

Mungu katika Utatu: Ukuu wa Mungu Sehemu ya 2: Sura Tatu za Utukufu wa Mungu: Utatu

Mch. Dkt. Don L. Davis

3

Mungu Baba Mwenyezi, ambaye mara nyingi hujulikana kama nafsi ya kwanza ya Utatu, anasifa zinazozungumza kwa nguvu na kwa uhakika kuhusu ukuu wake. Kwa kila njia, Mungu Baba ni roho, ana uzima ndani yake, ana haiba halisi, hana kikomo katika asili na tabia yake ya kiungu, na asili yake haibadiliki kamwe. Lengo letu katika sehemu hii, Sura Tatu za Utukufu waMungu: Utatu, ni kukuwezesha kuona kwamba: • Mungu Baba Mwenyezi ni Mungu na anazo sifa za kiungu za ukuu katika nafsi yake. • Baba Mwenyezi ni roho, hajaundwa kwa kitu wala kwa asili yoyote ya kimwili. • Mungu Baba Mwenyezi ni uzima na anao uzima, amekuwa hivyo daima na hawezi kuonja uharibifu wala mauti. • Mungu Baba Mwenyezi ni nafsi hai, anajitambua, ana uwezo wa kujua, kuhisi, na kuchagua, na anaweza kuhusiana na viumbe hai na uumbaji kwa ujumla.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

Made with FlippingBook - Share PDF online