Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

1 0 2 /

M U N G U B A B A

3. Ipi ni tafsiri ya sifa ya Mungu kama anayemiliki uzima ? Inamaanisha nini kusema kwamba Mungu Baba Mwenyezi “hawezi kufa”? Ni kwa njia gani tunaweza kusema uzima wa Mungu, usio na mwanzo wala mwisho, hauwezi “kuharibika”? 4. Orodhesha baadhi ya vipengele vilivyojumuishwa katika uelewa wa kwamba Mungu Baba Mwenyezi ni nafsi. Ni kwa namna ipi haiba ya Mungu inatofautiana na yetu? Haiba ya Mungu inadokeza nini kuhusu uwezo wake wa kuhusiana na viumbe hai vyenye ufahamu? 5. Ni kwa namna zipi tunaweza kusema kwamba asili ya Mungu Baba Mwenyezi haina ukomo? Kutokukoma kwa Mungu kukihusishwa na nafasi kunatuambia nini kuhusu Yeye? Vipi kuhusu kutokoma kwake kukihusishwa na wakati ? Vipi kuhusu kukoma kwake kukihusishwa na ujuzi au ufahamu? Vipi kuhusu kukoma kwake kukihusishwa na uwezo ? 6. Inamaanisha nini kusema kwamba Mungu Baba Mwenyezi habadiliki na ni wa kudumu? Je, Mungu hubadili mawazo yake kwa namna yoyote hata kidogo? Kama ndivyo, ni kwa namna gani? Kwa nini ni muhimu kusisitiza asili ya kutobadilika kwa Mungu hasa kuhusiana na maagano na ahadi zake? Kuhusu upendo wake kwa wanadamu? Kuhusu kusudi lake la kuokoa? 7. Ni kwa namna gani tunaweza kuzielewa sana sifa za ukuu wa Mungu kwa pamoja kiasi ambacho tukawa na uwezo wa kuzifahamu kila moja katika mwangaza wa nyingine? Unaweza kupendekeza namna ambayo tunaweza kuelewa sifa hizi kuu zenye utukufu kwa pamoja badala ya kila moja peke yake? Somo hili linajikita katika asili ya Utatu mtakatifu na sifa za ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi. Fundisho la Utatu linathibitisha madai ya Maandiko kwamba Mungu ni mmoja na bado yuko katika nafsi tatu tofauti, ambazo zote zinarejelewa kama Mungu, na zinashiriki utukufu wa asili ya uungu. Mungu Baba, nafsi ya kwanza ya Utatu, anazo sifa zinazozungumza kwa nguvu na kwa uhakika kuhusu ukuu wake. Kama Mungu Baba alivyo roho, anao uzima ndani yake, haiba yake ni halisi, hana ukomo katika asili na tabia yake ya kiungu, na ana uhalisia usio badilika. ³ Fundisho la Utatu hurejelea fundisho la Biblia kuhusu utatu wa nafsi ya Mungu.

3

MUUNGANIKO

Muhtasari wa Dhana Muhimu

Made with FlippingBook - Online catalogs