Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 1 0 1
M U N G U B A B A
a. Baadhi ni anthropomorphisms.
b. Mungu anaweza kutekeleza mipango yake katika awamu kadhaa mabazo kwetu ikaonekana kama kubadili nia (k.m., kutoa wokovu kwa Mataifa).
c. Mungu huitikia mabadiliko ya wanadamu (k.m., toba ya Ninawi katika Kitabu cha Yona).
Hitimisho
» Mungu Baba Mwenyezi ni mtukufu katika ukuu wa uungu wake.
» Sifa zake zinazohusiana na ukuu zinahusisha hali yake ya kiroho, uzima wake, haiba yake, asili yake ya kutokoma, na asili yake ya kutobadilika.
3
Sasa ni wakati wako tena wa kupitia dhana muhimu zinazohusiana na maarifa ya sehemu ya pili ya video. Ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi hauwezekani kueleweka, na nia hasa ya sehemu hii ilikuwa ni kukupa muhtasari wa jumla wa “sifa za asili” zinazohusishwa na ukuu wa Mungu, utukufu na adhama yake isiyo na kifani. Unapojibu maswali yafuatayo, hakikisha unatoa majibu yaliyo kamili, ukitafuta kuelewa dhana za msingi ambazo zimeungamanishwa kila moja na nyingine. Jitahidi kuwa wazi katika majibu yako ya maswali haya na hakikisha kwamba unatumia Neno la Mungu kujenga hoja na kuthibitisha kila hitimisho lako. 1. Nini maana ya neno ukuu linapohusianishwa na nafsi ya Mungu Baba Mwenyezi? Je, ni nini hasa sifa za kiungu za ukuu zinadokeza kuhusu asili ya tabia na nafsi ya Baba? 2. Maandiko yanafundisha nini kuhusu asili ya kiroho ya Baba Mwenyezi? Yeye akiwa roho, tunajua nini basi kuhusu asili ya Mungu ambacho hakipo kwa viumbe wengine? Ni kwa namna gani asili ya Mungu kama roho inatofautiana au kufanana na ile ya malaika?
Sehemu ya 2
Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook - Online catalogs