Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

1 0 4 /

M U N G U B A B A

Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafuzi wenzako maswali yako mwenyewe magumu kuhusu Utatu na sifa za kiungu za ukuu wa Baba. Bila shaka unayo maswali kadha wa kadha ambayo yamekuja akilini ulipokuwa ukisikiliza, ukijifunza, ukiomba, na kutafakari mada hizi kuu za Neno la Mungu. Chukua muda, kukusanya maswali yako mwenyewe kuhusu mada hizi na nyingine zinazofanana nazo, na uwashirikishe wanafunzi wenzako. Shirikianeni kwa pamoja juu ya mambo yaliyojitokeza katika kusoma kwenu somo hili. Pengine maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kuwaongoza katika mielekeo tofauti. * Je, mtu anaweza kuwa Mkristo na bado akalikataa fundisho la Utatu? Ni fundisho la muhimu kama lile la wokovu kwa neema kwa njia ya imani, au mtu anaweza kuwa na mtazamo tofauti juu ya Mungu na bado akachukuliwa kuwa mwamini wa kweli? * Kwa kuwa neno “Utatu” lenyewe halipo katika Biblia, theolojia inawezaje kulifanya kuwa “fundisho muhimu” la imani? * Je, mtu anaweza kuamini jambo fulani kuhusu Mungu kama vile Mashahidi wa Yehova wanavyoamini (Mungu Baba pekee ndiye Mungu; Yesu ni wa pili kwa ukuu na ameumbwa na Mungu na Roho Mtakatifu ni nguvu ya Mungu kwa ajili ya huduma) na bado akachukuliwa kuwa sawa kibiblia? Ikiwa ndiyo, kwa nini? Kama siyo, kwa nini? * Unawezaje kuuelewa sana ukuu wa Mungu hadi ukaathiri kila ufanyalo: ibada, mwenendo na tabia, na huduma yako? Unawezaje kuufanya ukweli huu mkuu kuwa maisha yenye nguvu kwa ajili ya Mungu? * Wengi humtazama Mungu kama anayetaka kukidhi mahitaji yao, na si kama Mungu katika Utatu na mkuu wa ulimwengu. Unawezaje kubadili mtazamo huu kutoka kumtazama Mungu kama aishiye kwa ajili yangu hadi kumtazama Mungu kama ambaye kwake vitu vyote vimepata kuwepo? * Ni njia zipi zinazoweza kuwasaidia kwa vitendo waamini wanaokua kutamani na kujifunza “kweli za ndani zaidi” za Neno la Mungu kuhusu sifa, tabia, na jina la Mungu? * Sifa za ukuu wa Mungu (yaani, hali yake ya kiroho, uzima, nafsi, kutokoma, na kudumu kwake) huzungumza kuhusu yeye kuwa juu kabisa ya ufahamu wetu. Je, ni kwa jinsi gani imani yetu katika Yesu Kristo inatufanya tuweze kumfikia Baba zaidi (rej. Yoh. 1:18; Yoh. 14:7-9)?

Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi

3

Made with FlippingBook - Online catalogs