Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 1 0 5
M U N G U B A B A
MIFANO
“Hayaonekani Kuwa Muhimu”
Wakati wa mfululizo wa somo la sifa za Mungu katika mafundisho ya Biblia ya Mchungaji katikati ya juma, mwamini mchanga mwenye njaa, anainua mkono wake na kutoa maoni kuhusu somo hilo. “Mchungaji,” anasema kama mwenye kutoa utetezi, “Ninajua kwamba hii inaweza kuwa muhimu katika mazingira ya seminari, lakini kiukweli, ninapata shida kuona kwa nini tunapaswa kujifunza maneno na vitu vyote vinavyochekesha kuhusu Mungu. Tuna haja gani ya kuelewa yale ambayo Wakristo waliyaamini zamani kabisa huko kuhusu asili ya Mungu, au kutumia maneno mengine yoyote kama ousios or homousia au maneno yoyote magumu ya aina hiyo. Nataka tu kujua habari za Yesu, kwa kweli sijali sana kuhusu fundisho hata hivyo. Je unaweza kuniambia ni kwa nini, mimi kama mwamini mchanga, natakiwa kupendezwa na mambo yote haya, kwangu hayaonekani kuwa muhimu sana, wala hayaonekani kuendana na jambo lolote ninalofanya.” Kama mchungaji, ungejibuje swali hili linaloulizwa na dada huyu mpendwa katika Kristo? Mwinjilisti/mhubiri maarufu wa televisheni amejitokeza hivi karibuni na mtazamo wa utatu ambao umeleta mkanganyiko mkubwa katika jamii za Kikristo. Badala ya kuthibitisha maoni ya kimapokeo ya Kikristo kuhusu Utatu kuwa Mungu mmoja anayejidhihirisha katika nafsi tatu tofauti (Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu), mwalimu huyo maarufu anaamini kwamba kuna Mungu mmoja ambaye kwa kweli hujionyesha katika namna tatu kutegemeana na hali na mazingira. Kwa maneno mengine, wakati anathibitisha kwamba Mungu ni mmoja, anapinga utofauti wa nafsi za Utatu. Kuna Mungu mmoja tu anayejidhihirisha katika namna tatu tofauti. Kwa nini mtazamo huu haukubaliki kulingana na Neno la Mungu? Je, ungeutazama mtazamo huu kuwa uzushi na upotofu? Kama ndiyo, kwa nini? Ikiwa siyo, kwa nini? Nyimbo nyingi sana za sifa na kuabudu leo zinaangazia ukaribu na uhusiano binafsi ambao mwamini anao sasa na Mungu. Nyimbo nyingi zinamzungumzia Mungu kama rafiki, msiri, hata kama mpenzi, zikiweka msisitizo katika kina binafsi cha uhusiano wetu na Mungu. Hata hivyo, ni wazi kwamba kwa kukosekana kwa fundisho thabiti katika mengi ya makanisa yetu, na kwa nyimbo za tenzi kupunguzwa kuimbwa kwenye mikusanyiko mingi, waamini wengi hawana ufahamu wa sifa za ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi . Katika uhalisia, Mungu wa makanisa mengi ni mkubwa kiasi cha kuweza tu kukidhi haja za mioyo yetu, Mungu Mmoja, katika Namna Tatu “Urafiki Usio na Afya”
1
3
2
3
Made with FlippingBook - Online catalogs