Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
1 0 6 /
M U N G U B A B A
si kushughulikia matatizo ya ulimwengu, achilia mbali kuukomboa ulimwengu katika hali yake ya kutoweza dhibitiwa. Kama mtu mmoja aliyewahi kuliongelea hili alivyosema: “Mungu wa makanisa mengi ni rafiki mwema, lakini haonekani kuwa Mungu Mkuu na Mwokozi wetu, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunaokena kuwa na urafiki usio na afya naye ambaye ni moto ulao.” Fikiria kwamba Bwana amekuita kuwa mhudumu wa muziki na ibada katika kanisa. Orodhesha misisitizo au vitu nane tofauti ambavyo ungefanya kuwasaidia waamini katika kanisa lako kupata uelewa mkubwa, wa thamani, na wa kibiblia wa ukuu wa Mungu katika ibada na maisha kwa ujumla. Fundisho la Utatu ni funidisho la kibiblia linalosema kwamba asili ya Mungu ni umoja wa nafsi tatu zinazoshiriki kiini kimoja kama Mungu. Biblia inasisitiza kwamba Mungu ni mmoja (Kum. 6:4), na Mungu huyu mmoja yuko katika nafsi tatu tofauti lakini zenye usawa, za milele, kila moja inatajwa kama Mungu katika Maandiko, na zinatajwa kushiriki utukufu wa asili ya kiungu. Utatu Mtakatifu (yaani, Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu) ni jina linalotolewa ili kuthibitisha madai ya Maandiko yenyewe ya umoja, utofauti, na usawa wa washiriki wa Uungu mmoja. Mungu Baba Mwenyezi, nafsi ya kwanza ya Utatu, anazo sifa zinazozungumza kwa nguvu na kwa uhakika kuhusu ukuu wake. Kama Mungu, Baba ni roho, ana uzima ndani yake, haiba yake ni halisi, hana ukomo katika asili na tabia yake ya uungu, na habadiliki katika asili yake. Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo juu ya asili ya Utatu na ukuu wa Mungu Baba Mwenyezi, unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo (tahadhari: huu si usomaji rahisi!): Charnock, Stephen. The Existence and Attributes of God. Grand Rapids: Baker Book House, 1996. O’Collins, Gerald, S. J. The Tripersonal God: Understanding and Interpreting the Trinity. Mahwah, NJ: Paulist Press, 1999. White, James R. The Forgotten Trinity: Recovering the Heart of Christian Belief. Bloomington, MN: Bethany House Publishing, 1998.
Marudio ya Tasnifu ya Somo
3
Nyenzo na Bibliographia
Made with FlippingBook - Online catalogs