Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 1 3 7
M U N G U B A B A
b. Je, asili ya Mungu inaashiria mvutano ndani ya nafsi yake, na kwa hiyo katika jinsi anavyohusiana na uumbaji wake?
B. Asili ya Mungu ni moja na yenye mwafaka kamili ndani yake.
1. Mungu ni mmoja; asili yake ni jumuishi na kamili.
a. Mungu wetu ni mmoja (kama Mungu pekee na aliye umoja ndani yake), Kum. 6:4.
b. Sifa zake zote zimejumuishwa katika nafsi yake na matendo yake, Kum. 4:35.
2. Sifa za Mungu zinaweza kuelezewa kila moja peke yake, lakini Mungu hutenda kazi katika ukamilifu wake na mapenzi yake.
4
a. Mungu anapotenda kwa upendo, mara zote ni upendo wenye haki; Mungu anapoifunua haki yake, mara zote ni haki yenye upendo.
b. Upendo pasipo haki = mihemko; haki pasipo upendo = ukatili
3. Mivutano hutokea kutokana na uchambuzi wa kimantiki wa sifa za Mungu.
a. Tabia ya uchambuzi unaopelekea utengaji au upunguzaji.
b. Kutokuwa na uwezo wa kuona kwamba sifa zote zimejumuishwa katika nafsi na tabia ya Mungu.
Made with FlippingBook - Online catalogs