Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 1 9 5
M U N G U B A B A
Tahariri (muendelezo)
walioifuata sheria ya haki, hawakuipata… Kwa nini? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo” (Rum. 9:32). Paulo hakuwa akisema utamaduni wa kidini wa Kiyahudi ulikuwa na kasoro au kwamba utamaduni wa Kiyunani ulikuwa bora zaidi. Alikuwa akisisitiza kwamba imani ya moyo ni kipengele muhimu katika utamaduni wowote – kwamba mifumo haikuwa jambo kuu bali imani . Wayunani walioipokea Injili kwa imani ya mioyo yao hawakuhitaji kuwa Wayahudi kitamaduni na kufuata mifumo ya Kiyahudi. Kama matokeo Paulo anasema, “Ninajivunia sana Injili ambayo ni nguvu ya Mungu ya kuwaokoa watu wanaomtii kwa imani, bila kujali wanafuata desturi za Kiyahudi au za Kiyunani” (Rom. 1:16). Lakini ujanja wa kweli sio tu watu wa imani katika kila utamaduni kukaa na kudumaa katika tamaduni zao mfu, bali ni kudumisha tamaduni zao na wakati huo huo kutambua uhalali wa miundo mbalimbali ya kiimani ndani ya tamaduni zingine na katika ujumla wa Mwili wa Kristo. Vyanzo tofauti vya Ukristo wa Ulaya vilitiririka hadi Mrekani, vikizalisha “ladha” 200 tofauti za Ukristo – baadhi zilizaliwa hapa (Wamormoni, Mashahidi wa Yehova) nyingine zikiwa za kibiblia, na nyingine za kiajabuajabu sana. Jambo sawa na hilo hutokea kwenye uwanja wa umisheni: mielekezo mingi tofauti huibuka. Kinachofaa ni Injili kudhihirishwa kwa ufanisi ndani ya lugha na tamaduni za watu na sio tu kufanyika kama upandikizaji wa utamaduni wa wamishenari. Kitabu maarufu cha H. Richard Niebhur’s, Social Sources of Denominationalism, kinajulikana kwa kuonyesha kwamba madhehebu mbalimbali hayakuwa tu na tofauti za kimafundisho (mara nyingi ni ndogo sana) lakini kwa kawaida yaliakisi, angalau kwa muda, tofauti za kijamii ambazo ndizo zilileta utofauti halisi. Kumbuka, hata hivyo, imani ya Kikristo mara nyingi ilikuwa “Harakati za Ndani” na ilidhihirishwa katika mikondo tofauti ya kijamii, ikichukua tabia za mikondo hiyo tofauti. Lakini, tukirejea kwenye umisheni: Suala la Uyahudi/Uyunani ni “baya zaidi” na zaidi kuliko tofauti kati ya Wamethodisti wanaoomba kwamba makosa yao yasamehewe na Wapresbiteri wanaoomba wasamehewe deni zao! Hapana, katika siku za Paulo tohara ilikuwa kizuizi kikubwa kwa wanaume watu wazima wa Kiyunani kuwa wafuasi wa Kristo wenye kuzikubali tamaduni za
Made with FlippingBook - Online catalogs