Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

1 9 6 /

M U N G U B A B A

Tahariri (muendelezo)

Kiyahudi. Jambo lingine nyeti lilikuwa ni suala la kula nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu, na kadhalika. Baadaye katika historia, mvutano wa Wayahudi na Wayunani ulilinganishwa na mvutano wa Walatini na Wajerumani. Wakati huu, tunaona tofauti kubwa katika mtazamo kuhusu ndoa kwa makasisi dhidi ya useja na matumizi ya Kilatini katika huduma za kanisa. Kwa karne nyingi Kilatini kilikuwa lugha ya Ulaya, kikawawezesha mawaziri, mawakili, madaktari, na maofisa wa umma kusoma vitabu vya taaluma zao katika lugha moja. Hilo lilidumu kwa muda mrefu! Kwa karne nyingi lugha ya usomaji yenye kuunganisha watu ilikuwa na faida nyingi nzuri. Lakini Biblia haikupata mafanikio makubwa hadi ilipotafsiriwa katika lugha ambazo ndio moyo hasa wa lugha za Ulaya. Matumizi makubwa ya Biblia ndiyo hasa yaliyoleta ustaarabu na usasa katika bara la Ulaya. Ni jambo la kusisimua na labda la kusumbua – wazo kwamba imani ya kibiblia inaweza kuvikwa lugha yoyote na utamaduni wowote. Shuhudia ukweli wa kustaajabisha katika zile zinazoitwa leo hii nchi za kimisheni. Iwe Afrika, India, au Uchina, inaweza kuwa kwamba idadi kubwa zaidi ya waamini wa kweli wa Yesu Kristo hawaonekani katika yale ambayo kwa kawaida tunayaita makanisa ya Kikristo! Unaweza kuamini hilo ? Bado wanaweza kujiona kuwa Waislamu au Wahindu (katika maana ya kitamaduni). Ni jambo baya kwamba leo hii Ukristo wenyewe unatafsiriwa kwa misingi ya kitamaduni ya ustaarabu wa Magharibi. Watu katika nchi za kimisheni ambao hawataki kuwa “wa kimagharibi” wanahisi wanahitaji kukaa mbali na Kanisa la Kikristo, ambalo katika nchi yao wenyewe mara nyingi linatafsiriwa kama la kimagharibi kwa maana ya utamaduni wake, theolojia, na tafsiri ya Biblia nk. Kwa mfano, huko Japani kuna “makanisa” ambayo ni ya kimagharibi kiasi kwamba katika miaka arobaini iliyopita hayaongezeki hata kwa mshirika mmoja. Wachunguzi na wakaguzi wengi wamehitimisha kwamba bado hakuna “aina ya Ukristo wa Kijapani.” Na pengine itakapojitokeza, haitataka kujihusisha na mapokeo ya Kikristo ya Magharibi isipokuwa kwa maana tu ya kujenga uhusiano wa udugu katika Kristo.

Made with FlippingBook - Online catalogs