Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 1 9 7

M U N G U B A B A

Tahariri (muendelezo)

Katika India sasa tunajua kwamba kwa kweli kuna mamilioni ya Wahindu ambao wamechagua kumfuata Kristo, wakisoma Biblia siku zote na kuabudu katika ngazi ya kaya, lakini si mara nyingi wanaotembelea makanisa ya Kikristo yanayohusiana na mambo ya Magharibi. Katika baadhi ya maeneo maelfu ya watu wanaojiona kuwa Waislamu ni wafuasi wa Yesu Kristo wa moyo na nafsi kabisa na hubeba Agano Jipya wapoingia misikitini. Katika Afrika kuna waamini zaidi ya milioni 50 (wa aina fulani) ndani ya duru kubwa iitwayo “Makanisa ya Kitamaduni ya Afrika.” Watu katika “Kanisa Rasmi la Kikristo” wanaweza wasiwachukulie hawa wengine kama Wakristo hata kidogo. Hakika, baadhi yao wako mbali zaidi na imani sahihi ya kibiblia kuliko Wamormoni. Lakini, ikiwa wanaheshimu na kujifunza Biblia, tunahitaji kuiacha Biblia ifanye kazi yake. Vikundi vya aina hii ni vile vyenye uzushi na upotofu wa hali ya juu na vingine vikiwa na umakini wa kibiblia ambavyo kwa ujumla wake vinaunda “madhehebu” zaidi ya elfu kumi ambayo hayahusiani na kikundi chochote rasmi cha Kikristo. Kwa hivyo, si harakati zote za “ndani” zinafaa. Ukristowetuwenyewe haujafanikiwa sana “ndani” ya utamaduni wetu, kwani “Wakristo” wengi ni Wakristo kwa jina tu. Hata shughuli za utume za “upandaji makanisa” zinaweza kuwa au zisiwe “za ndani” hata kidogo, na hata zikiwa hivyo zinaweza zisiwe sahihi. Ulimwenguni kote badhi ya harakati hizi hazibatizi watu. Katika mazingira mengine hubatiza. Nimeulizwa, “Je unachochea wazo la waamini wasiobatiza?” La hasha! Katika kuripoti kuwepo kwa mamilioni ya watu hawa, tunaripoti juu ya uwezo wa ajabu wa Biblia. Hatuendelezi mawazo yoyote wanayoakisi au mazoea wanayofuata. Biblia ni kama moto wa chini ya ardhi unaowaka usiweze kudhibitiwa! Kwa namna fulani tuna sababu ya kufurahi sana.

Made with FlippingBook - Online catalogs