Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
1 9 8 /
M U N G U B A B A
K I A M B A T I S H O C H A 2 7 Neno “Mkristo” Linaposhindikana Kutafsiri Frank Decker
Makala haya yamechukuliwa kutoka Mission Frontiers: The Bulletin of the US Center for World Mission, Buku la 27, Na. 5; Septemba-Oktoba 2005; ISSN 0889-9436. Copyright 2005 ya taasisi ya U.S. Center for World Mission. Yametumiwa kwa idhini. Haki Zote Zimehifadhiwa.
“Nilikua kama Muislamu, na nilipotoa maisha yangu kwa Yesu nikawa Mkristo. Kisha nikahisi Bwana akisema, ‘Rudi kwa familia yako uwaambie kile ambacho Bwana amekutendea.’” Huo ndio ulikuwa mwanzo wa ushuhuda wa dada mzuri katika Kristo aitwaye Salima. Aliposimama mbele ya kipaza sauti kwenye mkutano uliofanyika hivi majuzi huko Asia, nilifikiri jinsi ambavyo hadithi yake ingeshangiliwa na marafiki zangu wa Kikristo kule nyumbani. Lakini baadaye alisema jambo ambalo pengine lingewashtua Wakristo wengi wa Marekani. Alituambia kwamba ili kuishirikisha familia yake habari za Kristo, sasa anajitambulisha kuwa Muislamu badala ya Mkristo. “Lakini”, aliongeza, “Nisingeweza kamwe kurudi kwenye Uislamu kama si kwa sababu ya Yesu ambaye ninampenda kama Bwana wangu.” Kama mwanamke huyu, watu wengi sana, hasa katika Asia, wanaoishi katika mazingira ya Kiislamu, Kibudha, na Kihindu wanasema ndiyo kwa Yesu, lakini hapana kwaUkristo. Kama watuwaMagharibi, tunadhani kwamba neno “Mkristo” ipso facto (kwa sababu hiyo) linarejelea mtu ambaye ametoa maisha yake kwa Yesu, na “asiye – Mkristo” ni asiyeamini. Hata hivyo, kwa maneno ya mshirika mmoja wa Asia, “Neno ‘Mkristo’ linamaanisha kitu tofauti hapa Mashariki.” Angalia kisa cha Chai, Mbudha kutoka Thailand. “Thailand haijawahi kuwa nchi ya Kikristo, kwa sababu machoni pa Wathai, kuwa Mkristo inamaanisha huwezi kuwa Mthai tena. Hiyo ni kwa sababu nchini Thai ‘Mkristo’ ni sawa na ‘mgeni’.” Kwa hiyo Chai alipotoa maisha yake kwa Yesu, alianza kujiita “Mtoto wa Mungu” na “Mbuddha mpya.” Kisha akasimulia kisa kilichofuata ambapo alikuwa na mazungumzo na mtawa wa Kibuddha kwenye gari-moshi. “Baada ya kusikiliza hadithi yake, nilimwambia kwamba alikuwa akikosa kitu kimoja maishani. Akaniuliza nini hicho nikamwambia ni Yesu.” Chai aliendelea kutusimulia kisa ambacho mtawa yule si tu kwamba alitoa maisha yake kwa Kristo, bali pia alimwalika Chai aje kwenye hekalu lake la Kibuddha ili kuzungumza habari za Yesu. Kisha Chai akasema, “Mwanzoni mwa mazungumzo yetu yule mtawa aliniuliza, ‘Wewe ni Mkristo?’ na nikasema hapana. Nilimuelezea kwamba Ukristo na Yesu ni mambo mawili tofauti. Wokovu umo ndani ya Yesu,
Mmishenari wa Zamani nchini
Ghana, Decker sasa anahudumu kama Makamu wa Rais wa Opereresheni za “Shambani” za Jumuiya ya Kimisheni ya Muungano wa Wamethodisti.
Made with FlippingBook - Online catalogs