Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 1 9 9
M U N G U B A B A
Neno “Mkristo” Linaposhindikana Kutafsiri (muendelezo)
sio katika Ukristo. Kama ningelisema nilikuwa ‘Mkristo,’ mazungumzo yangeishia papo hapo.” Lakini hayakwisha. Na mtawa huyu sasa anatembea na Yesu. Hakika mmishenari wa Kimerekani ambaye amekuwa akifanya kazi huko Asia kwa takribani miongo miwili alisema, “kwa miaka mitano au saba ya huduma yetu katika [nchi ya Kiislamu] tulichanganyikiwa kwa sababu tulikuwa tunajaribu kuwafanya watu wabadili dini zao.” Aliendelea kusema jinsi gani katika duru za kiinjilisti tunazungumza sana namna ambavyo si dini yetu inayotuokoa, ni Yesu. “Ikiwa tunaamini hivyo kweli, kwa nini tunasisitiza kwamba watu wabadili dini zao?” Asif ni ndugu katika Kristo ambaye nimekaa naye kwa muda katika kijiji chake katika nchi ambayo asilimia 90 ni Waislamu. Mashirika ya Kikristo ya kimapokeo nchini humo yamekuwa na athari kubwa na njema kwa asilimia 10 nyingine ambayo haijawahi kuwa Waislamu. Usifikirie tofauti – Asif amejikita kweli kweli kwa Yesu, kama walivyo washirika wengine wa harakati za Waamini wenye Asili ya Uislamu – Muslim Background Believers (MBB). Sitasahau nilipoona machozi yakitiririka machoni mwa Asif aliponiambia jinsi yeye na kaka yake ambaye pia ni mwamini wa Yesu walivyopigwa katika shambulio ambalo kaka yake hakupona. Hawa ni Waislmu wanaotembea na Yesu na waziwazi wakiwashirikisha rafiki zao wa Kiislamu habari za Bwana, ambaye kwa Kiarabu anajulikana kama “Isa al Masih” (Yesu Masihi). “Harakati hizi za ndani” hazikusudiwi kuuficha utambulisho wa kiroho wa mwamini, bali kuwawezesha wale walio ndani ya harakati hizo kuingia ndani kabisa ya utamaduni wa jamii husika – iwe ya Kiislamu, Kihindu – na kuwa mashahidi wa Yesu katika muktadha wa utamaduni huo. Katika baadhi ya nchi, harakati kama hizo zimeanza hivi karibuni tu. Katika maeneo mengine, makadirio ya wafuasi ni mamia ya maelfu. Kama Mwili wa Kristo, tunapaswa kuwa waangalifu sana kwamba mambo tunayoyashikilia kuwa matakatifu yasiwe “makorokoro” ya baada ya wakati wa Biiblia, bali yawe kwa hakika mambo yale ya milele. Ikiwa hatuko wazi kwa viriba “vipya vya divai” tunaweza kujikuta tumeshikamana na mapokeo bila kujua, kama walivyokuwa Mafarisayo katika siku za Yesu.
*Majina katika visa hivi yamebadilishwa. Makala haya yametolewa kwa ruhusa kutoka toleo la May/Juni 2005 la Good News Magazine, huduma ya urejesho ndani ya Kanisa la Muungano wa Wamethodisti (www.goodnewsmag.org).
Made with FlippingBook - Online catalogs