Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 0 3
M U N G U B A B A
Kushika Imani, Sio Dini (muendelezo)
walivyowataka watu wa mataifa mengine kumkubali Kristo katika msingi wa utamaduni wa Kiyahudi, vivyo hivyo Warumi na Wajerumani na Wamarekani wamewashinikiza wale wanaomgeukia Kristo pia kuzigeukia tamaduni za wale wanaowaletea ujumbe. Hivyo basi, imani yetu imekuja kujulikana kimsingi kama kitu cha kitamaduni, dini iliyofungashwa katika miundo na mifumo ya kitamaduni ya kundi lililo na nguvu. Na kuanzia karne ya nne hivi na kuendelea imekuwa ikionekana kwa kiasi kikubwa kama kitu cha utamaduni wa Ulaya – kilichokamatwa na mababu zetu wa Ulaya na kuingizwa kwenye utamaduni tofauti kabisa na ule ambamo imani ilipandwa hapo kwanza. Wale wanaoongoka kuingia katika Ukristo, basi wanaonekana kama watu walioacha dini zao za kitamaduni na kuchagua kufuata dini na, kwa kawaida, mifumo mingi ya utamaduni wa Ulaya. Mara nyingi waongofu kama hao huchukuliwa kuwa wasaliti dhidi ya watu wao na njia zao. Ikiwa imani yetu ni “ni dini ya miundo na mifumo” tu, inaweza kuigwa lakini sio kuingizwa kwenye muktadha wa watu na jamii fulani , inaweza kuwa kwenye ushindani na miundo mingine ya dini lakini haiwezi kuakisiwa kupitia miundo hiyo kwa sababu kimsingi inatafuta kuchukua nafasi ya miundo hiyo. Lakini Ukristo wa Kibiblia sio mkusanyiko wa miundo ya kitamaduni. Japo Ukristo wa kitamaduni uko hivyo. Na tunachanganyikiwa katika mijadala yetu kwa sababu mara nyingi haijulikani wazi kama tunazungumzia Ukristo halisi wa kibiblia au wa dini ya jadi ya jamii za Magharibi ambayo pia huitwa Ukristo. Katika mojawapo ya vitabu vyangu (1979a) nimejaribu kutofautisha kwa kuandika Ukristo wa kibiblia kwa herufi kubwa “U” na ukristo wa kitamaduni kwa herufi ndogo “u”…. Binafsi…. ningeita dini kuwa kitu cha kimuundo, kielelezo kupitia miundo ya kina ya kitamaduni ya dhana na maana (mtazamo). Miundo ya kidini ni mahususi kwa utamaduni na, ikiwa dini imekopwa kutoka kwa muktadha mwingine wa kitamaduni, inahitaji aina fulani za utamaduni huo mwingine kukopwa pia. Uislamu, kwa mfano, unahitaji namna fulani za maombi, hija, kitabu cha Kiarabu kisichoweza kutafsiriwa, hata mitindo ya mavazi. Kadhalika Uyahudi, Uhindu, Ubudha na Ukristo wa kitamaduni. Hizi ni dini. Ukristo halisi wa kibiblia, hata hivyo, hauhitaji muundo wowote wa asili wa kitamaduni. Hiyo ndiyo sababu unavyoweza “kukamatwa” na watu wa Magharibi na kuchukuliwa kama ni wa Kimagharibi ingawa asili yake si Magharibi. Ukristo halisi ni utii, uhusiano, ambao kupitia huo hutiririka mfululizo wa maana zilizokusudiwa kuakisiwa kupitia miundo ya utamaduni wowote. Hivyo basi, miundo hii imekusudiwa
Made with FlippingBook - Online catalogs