Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 2 0 5

M U N G U B A B A

K I A M B A T I S H O C H A 2 9 Kuweka katika Muktadha Miongoni mwa Waislamu, Wahindu, na Wabudha: Kuangazia “Harakati za Ndani” John na Anna Travis

Makala haya yamechukuliwa kutoka Mission Frontiers: The Bulletin of the US Center for World Mission, Buku la 27, Na. 5; Septemba-Oktoba 2005; ISSN 0889-9436. Copyright 2005 ya taasisi ya U.S. Center for World Mission. Yametumiwa kwa idhini. Haki Zote Zimehifadhiwa.

John na Anna Travis, pamoja na watoto wao wawili, wameishi katika kitongoji cha Waislamu wa Kiasia kwa karibu miaka 20. Wanatumika katika kueneza habari njema, kutafsiri Biblia na huduma ya maombi ya uponyaji wa ndani kwa kuzingatia muktadha. Pia wamesaidia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi katika nchi za Asia, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Wote wawili wanasoma kwa ajli ya kupata shahada za juu, huku John akiwa mwanafunzi

Yafuatayo yamenukuliwa kwa idhini ya waandishi. Toleo kubwa la makala haya linapatikana katika sura ya 23 ya Appropriate Christianity (William Carey Library Publishers, 2005). Mengi yameandikwa kwa muda wa miaka 25 iliyopita juu ya matumizi ya muktadha katika huduma miongoni mwa Waislamu. Mnamo mwaka 1998 mimi (John) niliandika Makala ya Evangelical Missions Quarterly ambamo niliwasilisha kielelezo cha kulinganisha aina sita tofauti za ekklesia au makusanyiko (ambayo ninayataja kama “Jumuiya zenye msingi wa Kristo”) yanayopatikana katika ulimwengu wa Kiislamu leo (Travis 1998). Aina hizi sita za jumuiya zenye msingi wa Kristo zimetofautishwa katika misingi ya mambo matatu: lugha, miundo ya kitamaduni, na utambulisho wa kidini. Kielelezo hiki, kinachojulikana kama C1 – C6 (au mwendelezo wake), kimezua mjadala mkubwa, hasa kuhusu suala la ushirika wa “Waislamu ambao ni wafuasi wa Yesu” (nafasi ya C5 kwenye mizani). Parshall (1998), mtetezi wa dhana ya muktadha, anahisi kwamba C5 inavuka mpaka na kuangukia katika usawazishaji hatari. Katika maandiko yaliyofuata dukuduku nyingi za Parshall zimetatuliwa ( taz. Massey 2000, Gilliland 1998, Winter 1999, Travis 1998 and 2000). Licha ya maswali ambayo wengi wanaweza kuwa nayo juu ya suala hili, ukweli unabaki kwamba katika nchi kadhaa leo, kuna makundi ya Waislamu ambao kwa kumaanisha kabisa wanaifuata Imani ya Yesu Kristo, na bado kisheria na kidini katika muktadha wa jamii zao, wamesalia katika jamii za Kiislamu ….. Hatutaki kusisitiza kwamba C5 ndiyo bora au jambo pekee ambalo Mungu anafanya katika ulimwengu wa Kiislamu leo; hakika Mwenyezi Mungu anawaleta Waislamu kwake kwa namna nyingi sana, ambazo baadhi yake tutakuja kuzielewa katika umilele ujao. Tutakachoweka bayana, hata hivyo, ni kwamba njia mojawapo ambayo Mungu anatembea katika hatua hii ya historia ya wokovu, ni kwa kuwavuta Waislamu kwake mwenyewe, kufanya mapinduzi ya kiroho ndani yao, na kuwaita wabaki kuwa chumvi na nuru katika jamii ya dini walimozaliwa…

wa Shahada ya uzamivu (Ph.D).

Made with FlippingBook - Online catalogs