Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
2 0 8 /
M U N G U B A B A
Kuweka katika Muktadha Miongoni mwa Waislamu, Wahindu, na Wabudha (muendelezo)
Wahindu ambao kwa hakika walikuwa wakimwabudu na kumfuata Yesu kwa siri katika nyumba zao. Akijua kwamba kuna Wahindu wengi wanaomheshimu sana Yesu kama mwalimu, aliamua kujua ikiwa walikuwa wamemkubali Yeye kuwa Bwana na Mwokozi au tu kama mwalimu mkuu aliyeelimika. Jitihada zake zikawa msingi wa tasnifu ya shahada ya udaktari ambapo alihoji familia 80 kama hizo za Kihindu na Kiislamu katika eneo la Madras, India. Hoefer aligundua kwamba idadi kubwa ya familia hizi, ambazo hazijawahi kubatizwa au kujiunga na makanisa, kwa hakika zina uhusiano wa kweli na Kristo na huomba na kujifunza Neno lake kwa bidii. Hoefer anasema kwamba wengi wanataka ubatizo, lakini hawajawahi kuona ubatizo ambao haufungamani na ulazima wa kuwa mshirika rasmi wa kanisa fulani. Hitimisho lake, baada ya mchakato mkubwa sana wa mahojiano na uchambuzi wa takwimu, ni kwamba Madras kuna Wahindu na Waislamu 200,000 wanaomwabudu Yesu – kiasi ambacho ni sawa na jumla ya Wakristo katika mji huo! Ni jambo linalotia ufahamu kutambua kwamba miaka 200 iliyopita, William Carey aliwataja wafuasi wa Kihindu wa Yesu kuwa “Wahindu wa Kikristo.” Yaonekana hii ilitokana na uhusiano wenye nguvu katika akili za Wahindi (na yamkini William Carey) kati ya kuwa Mhindu na kuwa Mhindi (katika uhalisia wa maana, neno India linatokana na neno Hindia , nchi ya Wahindu). Badala ya Uhindu kuwa angalau karibu na zile imani za Mungu mmoja, wenyewe ni kinyume kabisa: wafuasi wanaweza kuabudu idadi yoyote ya miungu. Inaonekana kwamba uwazi huu unaruhusu nafasi ya kumwabudu Mungu wa Biblia pekee kama Mungu mmoja wa kweli ( ona maneno ya Yoshua katika Yoshua 24:14-15). Mapema miaka ya 1900, mwinjilisti wa Kihindi Sadhu Sundar Singh aligundua makundi ya “chini kwa chini” ya wafuasi wa Yesu miongoni mwa Wahindu. Alipokuwa akihubiri Injili huko Benares, wasikilizaji wake walimwambia kuhusu mtu mtakatifu Mhindu ambaye alikuwa akihubiri ujumbe huo. Singh alikaa usiku mzima nyumbani kwa mwanaume huyo na kusikia madai yake kwamba mfumo wake huo wa Ukristo wa Kihindi ulikuwa umeanzishwa zamani na mtume Tomaso, na sasa ulikuwa na washirika 40,000. Singh baadaye aliona ibada zao (pamoja na ibada, sala, ubatizo na ushirika) ambazo zilifanyika katika sehemu ambazo zilifanana kabisa na madhabahu na mahekalu ya Kihindu, kando na sanamu. “Sundar alipojaribu kuwashawishi kwamba walipaswa kujitangaza waziwazi kuwa Wakristo, walimhakikishia kwamba walikuwa wakifanya kazi yenye matokeo zaidi wakiwa wafuasi wa siri, wakikubaliwa kama watawa wa kawaida wa Kihindu, lakini
Made with FlippingBook - Online catalogs