Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 0 9
M U N G U B A B A
Kuweka katika Muktadha Miongoni mwa Waislamu, Wahindu, na Wabudha (muendelezo)
wakivuta akiliza watu kwenye imani ya kweli, huku wakijiweka tayari kwa ajili ya siku hiyo ufuasi wa wazi utakapowezekana” (Davey 1950:80) [ sic ]. Hivii karibuni, tulikutana na mwanaume mmoja akiwafikia Wabudha ambao miongoni mwao kuna mchanganyiko wa hali ya juu sana wa utamaduni na dini. Kwa mshangao wangu alikuwa amechukua mwendelezo wa C1-C6 na kuuingiza katika muktadha wa Kibudha. Ingawa inaonekana kuwa haiwezekani kwa Injili kustawi ndani ya Ubudha, je, panaweza pasiwe na na mamilioni ya Wabuddha ambao ni waumini kwa jina tu na ambao ni Wabuddha kwa sababu tu ya kuzaliwa na utaifa? Kama Kraft alivyosema (1996:212-213), mara kanuni hii ya “uaminifu wa kweli wa kiroho badala ya dini rasmi” inapoeleweka, “tunaanza kugundua uwezekano wa kusisimua wa kufanya kazi ndani ya tamaduni, tuseme, za Kiyahudi au Kiislamu au Kihindu au Kibuddha au kianimisti kuwafikia watu ambao kitamaduni watakuwa Wayahudi au Waislamu au Wahindu au waanimisti hadi mwisho wa siku zao lakini Wakristo katika uaminifu wa imani yao.” (Kumbuka: katika kitabu chake Kraft anamfafanua Mkristo ambaye ni mfuasi wa Kristo kwa herufi kubwa “M” dhidi ya mkristo wa taasisi za dini kwa herufi ndogo “m”). Yote haya yanatuelekeza wapi? Je, hakuna ibada ya waziwazi kwa miungu katika Uhindu wa kimapokeo? Ipo kabisa, lakini si miongoni mwa wafuasi hao wa Kristo wa Kihindu walioelezewa na Hoefer na Davey. Je, si kweli kwamba Waislamu wengi hukana kwamba Yesu hakufa msalabani? Ndiyo, lakini si kwa wale Waislamu tuliowajua ambao wameweka imani yao kwa Kristo. Je, si kweli kwamba Wayahudi wanafundisha kwamba Masihi bado anakuja? Ndiyo, lakini maelfu ya Wayahudi huenda katika masinagogi ya Kimasihi na kuamini, kama vile maelfu ya Wayahudi katika karne ya kwanza walivyoamini, kwamba kwa hakika Yeshua ndiye Mwana wa Daudi aliyengojewa kwa muda mrefu. Karibia tunafikia hitimisho kwamba Mungu anafanya jambo jipya kufikia mataifa haya yaliyosalia ( ta ethne ) yanayotawaliwa na Imani au dini kubwa. Ikiwa Bosch alipatia aliposema kwamba Imani katika Kristo haikukusudiwa kuwa dini, je inaweza kwamba tunashuhudia baadhi ya matunda ya kwanza ya harakati kubwa ambapo Yesu anasababisha Injili kulipuka nje ya “Ukristo”? Ambapo wale wanaomjua Yesu watabakia kuwa harufu nzuri ndani ya dini zao walimozaliwa, na hatimaye idadi ya wafuasi waliozaliwa mara ya pili itakuwa kubwa sana kiasi kwamba harakati za mageuzi kutokea ndani ya dini hizo zitazaliwa? Mchakato huo unaweza kuwa na mkanganyiko wa kitheolojia, lakini hatuoni njia mbadala. Ikiwa tunazitazama tamaduni na dini zote kama ngozi ya mtu
Made with FlippingBook - Online catalogs