Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 1 3
M U N G U B A B A
Watu Waliozaliwa Upya (muendelezo)
ni tofauti na bora kuliko utaratibu wa zamani, basi katika maamuzi ya ushirika huhamia kwenye Imani ya Kikristo. Mwitikio wa mnyororo unapita kwenye kitambaa cha kikabila. Makusanyiko huongezeka. Kwa ujumla, inaweza kusemwa kwamba kadiri vikundi vya kwanza kujiunga na Ukristo vinavyofikia viwango vya Ukristo vilivyo juu vya Imani ya Kikristo, ndivyo kielelezo chao kinavyokuwa na ushawishi mkubwa zaidi. Keysser, mfikiriaji huru, aliliona hili….
Kuanzisha Kusanyiko la Kweli
[Sababu nyingine] kwa nini wanazuoni wamisiolojia watafaidika kutokana na kitabu hiki ni misisitizo thabiti wa Keysser juu ya vipaumbele na wajibu wa mmishenari kuunda kusanyiko la Kikristo kutokana na vijiji na koo mbalimbali . Kwa hili haimaanishi kuwachukua watu binafsi, kama kokoto zilizotengana, na kuwafanya kuwa shirika jipya linaloitwa kanisa. Badala yake, anamaanisha kuchukua ule muunganiko na mfumo wa kijamii, ambao kijiji au ukoo umefungamanishwa pamoja kwa msingi huo tangu zama zisizojulikana, na kwa kuusogeza mfumo au muunganiko huo kwenye mapenzi ya Mungu na Neno la Mungu, na kuuongoza kuishi na kutenda kwa kufuata mtindo wa Kikristo na kuugeuza kuwa kabila la Kikristo . Hili halifanyiki tu kwa kuubatiza. Kusikia Injili, kuiona Injili, kupokea maelekezo ya kutosha, baadhi yake kwa namna ya ajabu, kubatizwa kwa kibali cha ukoo, na kisha kwa miaka mingi wakiongozwa na mmishenari na Neno, wanawezeshwa kifikiria yale ambayo Kristo anataka kijiji, ukoo au kabila (kusanyiko la Kikristo) kutenda katika mazingira na matukio mahususi – hatua hizi zote zinahitajika ili kubadilisha vikundi vya kijamii visivyo vya Kikristo kuwa kutaniko la Kikristo…. Maoni hasi ya Dr. Keysser kuhusu makanisa nchini Ujerumani yanapaswa kuchukuliwa kama sehemu ya imani yake kuhusu Kanisa la Kweli. Katika kitabu hiki chote anakosoa makusanyiko nchini Ujerumani kwa kutokuwa jumuiya za kweli, yaani makusanyiko ya kweli. Mwaka 1922 Keysser aliporudi Ujerumani, alikumbana na mshtuko wa kitamaduni. Alikuta “makanisa” ambayo kama makanisa yalifanya kidogo sana kwa habari ya huduma ya kichungaji kwa washirika wao na pengine hayakufanya kabisa…. Makusanyiko hayakuwa jumuiya halisi.… Leo, wakati ambapo uanzishaji wa jumuiya zinazojali katika makanisa ya magharibi umekuwa mojawapo ya madhumuni makuu ya Ukristo wa kisasa, maoni ya Keysser kuhusu Kanisa la Ujerumani ni muhimu sana. Yanaweza kuthibitishwa kuhusu Kanisa katika mataifa mengi yaliyoendelea. Jamii inapokumbwa na migawanyiko, ubinafsi huzidi kutoweza kudhibitiwa na upweke huwatesa mamilioni ya watu.
Made with FlippingBook - Online catalogs