Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
2 1 4 /
M U N G U B A B A
Watu Waliozaliwa Upya (muendelezo)
Kanisa lazima lizalishe jumuiya zenye upendo, kujali na zenye nguvu. Maisha ni ya thamani kubwa zaidi yakiendeshwa kwa namna hiyo. Katika ulimwengu wa kale makanisa ya Agano Jipya yalikuwa jumuiya kama hizo. Makanisa yanaweza tena kuwa hivyo, New Guinea na New York, Tokyo na Berlin, na kwa kifupi, katika kila nchi. Makanisa ya Kweli ni jumuiya hai. . . . Profesa Keysser ameupa ulimwengu wa umisheni ufahamu mwingi ambao utakuwa na manufaa makubwa katika karne ijayo. Katika siku zake, makabila ya kianimisti yalikuwa yakimfuata Kristo kupitia harakati za makundi ya watu na kuunda jumuiya za kweli (makusanyiko) katika Ukristo. Katika karne ya ishirini na moja, tutaona makundi makubwa ya watu katika mataifa yanayoendelea na yaliyoendela yakigeukia Imani ya Kikristo bila mtengano wa kijamii. Watabaki kuwa jumuiya halisi wanapofanyika makusanyiko halisi. Misiolojia ya kisasa inapaswa kutambua mchango wa Christian Keysser.
Made with FlippingBook - Online catalogs