Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 2 1 5
M U N G U B A B A
K I A M B A T I S H O C H A 3 1 Umisheni katika Karne ya 21 Kufanya Kazi na Wajasiriamali wa Kijamii? Rebecca Lewis
Makala haya yamechukuliwa kutoka Mission Frontiers: The Bulletin of the US Center for World Mission, Buku la 27, Na. 5; Septemba-Oktoba 2005; ISSN 0889-9436. Copyright 2005 ya taasisi ya U.S. Center for World Mission. Yametumiwa kwa idhini. Haki Zote Zimehifadhiwa.
Changamoto ni hii: inawezekanaje kuchochea “harakati za ndani” kwa Kristo katika jami ambayo hairuhusu kazi ya kimisheni katika mfumo wa kawaida? Ili hili litokee, Injili inahitaji kuenea kupitia mitandao ya kijamii iliyopo, ambayo inakuwa “kanisa.” Watu hawapaswi kutolewa kwenye familia zao au jumuiya zao na kuingia katika mifumo mipya ya kijamii ili kuwa waamini. Mungu anaonekana kufungua njia mpya ya fursa katika jamii zilizofungwa kupitia kufanya kazi na mawakala wa mabadiliko katika jamii– wajasiriamali wanaofanya kazi kuleta mageuzi ya kijamii. Kihistoria, mtindo uliofanikiwa zaidi wa kufikia mabadiliko ya kudumu ya kijamii umekuwa si serikali wala shughuli za kibiashara bali jamii yenye utayari wa kujitolea (pia inajulikana kama “sekta ya kiraia” au “jumuiya ya kiraia”). Wazo la wananchi kuungana pamoja ili kuleta mageuzi katika jamii lilichukua hatua kubwa mbele wakati wa Uamsho wa Kiinjili, ulioanzishwa na John Wesley katika karne ya 18. Kutokana na uamsho huu, na Uamsho mkuu wa pili mwanzoni mwa karne ya 19, kuliibuka mamia ya vyama au mashirika ya kujitolea, visivyofungamana na dhehebu moja. Vikiwa vimeanzishwa na wajasiriamali wenye maono ya kijamii, kila chama au shirika lilishambulia suala fulani, iwe ni kukomesha utumwa au kuanzisha shule maalum za Jumapili kuwafundisha kusoma watoto waliofanya kazi juma zima. Kwa nini tusitumie kielelezo hiki chenye mafaniko kuwa chombo cha kuendeleza makusudi ya Mungu miongoni mwa vikundi vya watu ambavyo havijafikiwi kikamilifu? Leo hii milango iko wazi katika nchi nyingi kwa watu ambao wanaweza kuanzisha shughuli za umma kushughulikia matatizo ya kijamii. Katika miaka ya 1990 idadi ya mashirika ya kimataifa yasiyo ya faida iliongezeka kutoka 6000 hadi 26,000, kiwango cha ukuaji cha zaidi ya asilimia 400. Kadhaika, mamia ya maelfu ya mashirika ya kitaifa yasiyo ya kiserekali (NGOs) yameundwa katika nchi zisizo za magharibi. Kwa nini ukuaji wa ghafla? Kwanza, tangu kuanguka kwa Muungano wa Sovieti, serikali nyingi zimekuwa zikiachia udhibiti wa uchumi na kukuza sekta binafsi. Pili, wajasiriamali wa kijamii na sekta ya asasi za kiraia sasa wanatambulika kwa kiasi kikubwa kutokana na mafaniko yao katika kutatua matatizo yaliyokuwa hayawezi kutatulika.
Rebecca Lewis alikaa Morocco kwa miaka minane kwenye timu ya upandaji makanisa na kwa sasa anatengeneza mitaala ili kuwasaidia vijana kuona jinsi wanavyoweza kuishi maisha yao kwa ajili ya makusudi ya Mungu.
Made with FlippingBook - Online catalogs