Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

2 1 6 /

M U N G U B A B A

Umisheni katika Karne ya 21: Kufanya Kazi na Wajasiriamali wa Kijamii? (muendelezo)

Tatu, serikali zinajikuta katika fedheha zaidi na zaidi pale zinapojaribu kuzuia shughuli na taasisi zisizo za faida kwa sababu kumekuwa na hali ya kimataifa ya uthamini wa “hisia-mwenzi” ( empathy ) ambayo imesababishwa na harakati za Kiinjili zinazoenea kwa kasi na kuingizwa kwa maadili ya Kikristo katika mifumo ya elimu ulimwenguni kote. Nne, kuna utayari mpya kwa ajili ya mabadiliko kiujumla. Kwa kadri watu katika maeneo ya mbali na fiche ya dunia wamefunguliwa macho kuuona ulimwengu kupitia vyombo vya habari, wanafikiria upya mifumo yao ya tabia na desturi za kitamaduni. Watu kila mahali wanaweka tumaini lao katika elimu na kuthamini maendeleo kuliko hapo awali. Kama matokeo, jamii katika maeneo yao, pamoja na serikali za kitaifa, zinarudi kusimama nyuma ya mashirika ya wananchi yanayotafuta kuleta ufumbuzi kwa matatizo ya kimfumo. Ikiwa lengo ni kuanzisha harakati za ndani kwa ajili ya Kristo, kwa nini ufanye kazi na wajasiriamali wa kijamii? Wafanyakazi wa Kikristo wanaweza kujenga uhusiano mpana na viongozi na familia ndani ya jamii kwa kuwasaidia wajasiriamali wa kijamii (kwamba ni waamini au la) kutimiza maono yao ya kushambulia tatizo fulani katika jamii yao. Aina hii ya uhusiano mpana wa kimtandao, ambayo huleta mabadiliko kwa jamii, huunda msingi bora wa uenezaji wa Injili kwa njia inayoongoza kwenye harakati za ndani. Kupitia kusaidia sekta ya kiraia, wafanyakazi wanajukumu linaloeleweka na la manufaa machoni pa watu na serikali ya eneo husika. Kama Yesu, wao pia wanaweza kutangaza Ufalme katika muktadha wa kuleta uponyaji katika jamii. Kwa wale ambao wangependa kujifunza zaidi kuhusu kutafuta na kusaidia wajasiriamali wa kijamii, ninapendekeza kitabu hiki cha kuvutia cha David Bornstein, How to Change the World: Social Entrepreneurs and the Power of New Ideas (Oxford University Press, 2003).

Made with FlippingBook - Online catalogs