Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
2 1 8 /
M U N G U B A B A
Kutoa Utukufu kwa Mungu (muendelezo)
B. Kumtukuza Mungu kunamaanisha kumtambua yeye kuwa chanzo chetu, umaana wetu, na usalama wetu katika jumla ya vile tulivyo na yale tunayofanya.
II. Mbingu na Nchi Ziliumbwa Ili Kumletea Mungu Utukufu.
Vitu vyote vilivyo na uhai na vilivyopo, iwe vinafahamu au la, viliumbwa kwa mkono wa Mungu ili kumpa utukufu. Ataupata kutoka kwetu, iwe kwa uzima, au kwa kifo, iwe kwa heshima au kwa njia ya msiba. A. Maandiko
1. Zab. 103:22 2. Zab. 145:10 3. Zab. 148:7-13 4. Mit. 16:4
5. Rum. 11:36 6. Flp. 2:9-11 7. Ufu. 4:11 B. Vielelezo na Kanuni
1. Ufunguo wa kuishi kwa ufanisi ni kuishi kwa kusudi ambalo Bwana alikuumba kuliishi, kuelewa wewe ni nani, na kwa nini Mungu amekuweka hapa. 2. Mtunga Zaburi anatangaza kwamba kila kitu chenye pumzi kinapaswa kumsifu Bwana, Zab. 150:6. 3. Katika siku za usoni zisizo mbali sana, Mungu anatangaza kwamba wanadamu wote kila mahali kwa hakika watamtambua Mungu kama chanzo, na kumpa utukufu anaostahili (Ufu. 5:12-14).
Made with FlippingBook - Online catalogs