Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

2 2 0 /

M U N G U B A B A

Kutoa Utukufu kwa Mungu (muendelezo)

4. Tumeitwa kumtukuza Mungu kwa matendo yake. a. Tunamsifu kwa alilolifanya : Kalvari b. Tunamsifu kwa analolifanya: Ukombozi. c. Tunamsifu kwa atakalolifaya : Ujio wa Pili C. Utukufu wa Mungu lazima uwe mkuu kwenye fahamu zetu.

1. Zaidi ya usalama wetu, Mdo 20:24 2. Zaidi ya urahisi wetu , Ebr. 12:2-3 3. Zaidi hata ya uzima wetu , Flp 1:20

Mungu anataka kutukuzwa ndani yetu bila kujalisha mazingira, tukiwa maskini au matajiri, tunapokuwa na furaha au huzuni, tukiwa na afya njema au wagonjwa. Ndiyo, Mungu anaweza hata kutukuzwa katika ugonjwa wetu! Ifuatayoni sala ya ajabu ya Mkristo mpendwa kutoka Norway, Ole Hallesby, ambayo inaakisi mtazamo mzima ambao Mkristo anapaswa kuwa nao kuhusu ugonjwa: “Bwana, ikiwa itakuwa kwa utukufu wako, ponya ghafla. Ikiwa itakutukuza zaidi, ponya taratibu, ikiwa itakutukuza wewe hata zaidi, mtumishi wako abakie mgonjwa kwa muda; na ikiwa italitukuza zaidi na zaidi jina lako, umchukue kwako mbinguni.”

IV. Kiini cha Dhambi ni Kushindwa Kumpa Mungu Anachostahili; Dhambi ni Kumwibia Mungu Utukufu Ambao ni Haki Anayostahili Yeye (Rum. 3:23).

Tunaweza Kumwibia Mungu Utukufu Angalau Katika Namna Nne

A. Kwanza, tunaweza kujitwaliwa wenyewe utukufu uliowekwa kwa ajili ya Mungu pekee.

1. Shetani, Isa. 14:13-20 2. Herode, Mdo 12:20-23 3. Vielelezo na Kanuni.

Made with FlippingBook - Online catalogs