Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

2 2 4 /

M U N G U B A B A

Kutoa Utukufu kwa Mungu (muendelezo)

V. Wito Mkuu wa kila Mkristo ni Kumtukuza Mungu katika Vyote Tulivyo, Yote Tusemayo, na Yote Tufanyayo, 1 Kor. 10:31. A. Tunapaswa kumtukuza Mungu katika miili yetu, 1 Kor. 3:16, 17; 6:19-20. 1. Usafi wa kingono. 2. Afya ya kimwili. B. Tunappaswa kumtukuza Mungu katika mawazo yetu, Rum. 8:5-8; 2 Kor. 10:3-5. 1. Mawazo zaidi ya 19,000 kwa siku, fikiria mara nne hadi tano haraka kadri mtu anavyoweza kuzungumza. 2. Uwanja wa vita wa mwisho wa maisha yako ni mawazo yako; kuwa makini na unachofikiria. 3. Mit. 23:7 C. Tunapaswa kumtukuza Mungu kwa maneno ya mazungumzo yetu, 1 Kor. 10:31; Efe. 4:29, Yak. 3:2. 1. Mtazamo huleta utofauti kabisa; Wakristo wengi humvunjia Mungu heshima katika mitazamo yao pengine kuliko kwa njia nyingine yoyote ile. 2. Mitazamo, iwe ni mizuri au mibaya, inaambukiza na ina athari. 3. Ulimi wako umeunganishwa na moyo wako. 4. Sio tu lugha chafu na matusi. 5. Mtazamo hasi na kejeli. 6. Kulalamika na kunung’unika. 7. Umbea na kusengenya. D. Tunapaswa kumtukuza Mungu katika mwenendo na tabia zetu, Mt. 5:16; Efe. 2:8-10. 1. Mungu anaweza kupokea utukufu kutokana na aina ya mambo unayoyafanya, matendo yako ya kila siku tu. 2. Tabia na sifa yako imefungamanishwa na sifa ya Kristo.

Made with FlippingBook - Online catalogs