Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
3 6 /
M U N G U B A B A
³ Kanuni ya Imani ya Nikea inatoa tamko la wazi kuhusu ukuu wa Mungu mmoja wa kweli, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. ³ Katika uhusiano wake na ulimwengu aliouumba, Mungu yupo katika uumbaji wake na yuko juu zaidi ya uumbaji na fahamu zote. ³ Uwepo wa Mungu katika uumbaji [immanence] unamaanisha uhusika wake wa sasa na hai katika uumbaji wake wote. ³ Sifa ya Mungu kuwa juu ya uumbaji na fahamu zote [transcendence] inarejelea ukweli kwamba Mungu hana ukomo na kwa hiyo hawezi kutoshea katika uumbaji au kujulikana pasipo uchaguzi wake mkuu wa kujifunua kwa wengine. ³ Sifa za Mungu zinarejelea sifa za Uungu Mtakatifu katika ukamilifu wake, yaani Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, na zinaweza kugawanywa kwa misingi ya ukuu wake na wema wake. ³ Sifa zinazohusiana na ukuu wa Mungu zinahusisha hali yake ya kiroho, uzima, haiba, kutokuwa na ukomo, na kudumu. ³ Sifa zinazohusiana na wema wa Mungu zinahusisha utakatifu wake, ukamilifu, na upendo. Sasa ni wakati wako wa kujadiliana na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu somo hili la utangulizi juu ya Fundisho kuhusu Mungu. Una maswali gani hasa kwa kuzingatia maarifa uliyojifunza hivi punde? Pengine baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako meenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Inaleta tofauti gani kusisitiza kwamba Mungu Baba Mwenyezi ndiye Muumba wa mbingu na nchi, wa vitu vyote vinavyonekana na visivyoonekana, na si nguvu fulani tu? Unadhani ni kwa nini maaskofu wa kanisa walianza Kanuni ya Imani kwa ukiri huu? * Kwa nini tunapaswa kusisitiza kwa moyo wote kwamba hakuna mtu awezaye kumjua Mungu bila Mungu kuchukua hatua ya kwanza ya kukutana na mtu? Ikiwa ndivyo, Mungu anawezaje kumhesabia hatia mtu yeyote ambaye hakumjia na hakumfahamu, ikiwa ni lazima Yeye [Mungu] aanzishe uhusiano huo? * Nini hutokea mtu anapoweka msisitizo uliopitiliza kuhusu umuhimu wa ufunuo wa jumla kuliko umuhimu wa ufunuo maalum? Kwa upande
1
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
Made with FlippingBook - Online catalogs