Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
/ 3 7
M U N G U B A B A
mwingine, nini hutokea mtu anaposisitiza ufunuo maalum bila kuelewa nafasi ya Mungu katika ufunuo wa jumla? * Inaweza kuwa na maana gani kusema kwamba Mungu yupo katika mambo ya jamii iliyoathiriwa na uhalifu na vurugu za magenge? Ikiwa Mungu yupo katika hali kama hizi, tunautambuaje uwepo wake kati yetu? * Je, unaweza kuthibitishaje sifa ya Mungu kama aliye juu ya uumbaji na fahamu zote katika mazingira ya machafuko ya jamii nyingi za mijini bila pia kusema kwamba Mungu ameitelekeza miji? Mungu anawezaje kuwepo katika uumbaji na kuwa juu zaidi ya vyote katika mambo yanayoendelea mijini mwetu leo hii? * Fundisho la uwepo wa Mungu katika uumbaji na sifa yake kama aliye juu zaidi ya uumbaji linapaswa kutuathiri kwa namna gani tunapohudumu katika makanisa kwenye miji yetu? Ni kwa namna gani linapaswa kuathiri uelewa wetu wa ibada? Huduma kwa wanaoumia? Kukabiliana na hali ngumu katika jamii? Maisha na huduma zetu wenyewe? * Ni kwa namna gani mtu anaweza kufaidika zaidi na kujifunza sifa za Mungu pasipo kutazama jambo moja tu kuhusu Mungu huku akiyapuuza mengine? Ni sifa zipi zinahusiana na ukuu waMungu, na ni zipi zinahusiana na wema wa Mungu? * Je, maisha na huduma yako vinaonyesha unafahamu kwamba Mungu ni mjumuisho wa sifa zake zote za ajabu, au unatazama tu moja ya sifa zaidi ya unavyotazama zingine? Unawezaje kukabiliana na tabia hii ya kawaida katika utafiti wa kifundisho? Katika mazungumzo na mmoja wa marafiki zako ambaye mnamwamini Bwana pamoja, anaangazia shida fulani ambayo inaonekana kumpa shida kabisa katika fikra zake kwa habari ya Bwana na wokovu. Huku akisumbuliwa na wazo kwamba kuna mamia ya mamilioni ya watu ambao bado hawajasikia kuhusu kazi ya Mungu ya kuokoa katika Yesu, rafiki yako anakueleza kwamba anafikiri imani ya Kikristo si ya haki kabisa. “Sawa, nitakwambia kwamba Mungu amejifunua mwenyewe katika uzuri wa uumbaji – ni wa ajabu mno. Lakini bado nina shida; ikiwa ufunuo wa jumla hautoshi kumwongoza mtu amwamini Kristo, basi nini kitatokea kwa wale mamilioni ya watu ambao bado hawajasikia kuhusu Kristo? Je, wamehukumiwa kufa, kupotea milele? Ikiwa unahitaji ufunuo maalum ili kumfahamu Yesu, basi vipi kuhusu watu hao wote?” Utajibuje swali la rafiki yako? Vipi kuhusu Watu Wote Hao?
1
MIFANO
1
Made with FlippingBook - Online catalogs