Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

/ 4 5

M U N G U B A B A

Mungu kama Muumba Uangalizi na Utunzaji wa Mungu

S O M O L A 2

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kueleza namna mamlaka kuu ya Mungu, uangalizi na utunzaji wake unavyodhihirishwa juu ya viumbe vyote na historia. • Kuonyesha ni kwa jinsi gani “uangalizi na utunzaji waMungu” unamaanisha kwamba “Mungu anatimiza mapenzi yake makuu katika ulimwengu ambamo matukio yote yamepangwa na/au kuruhusiwa naye ili kutimiza makusudi yake kwa ajili yake na uumbaji wake kwa kusudi jema.” • Kutumia Maandiko kuonyesha namna Baba alivyo Mkuu juu ya yote, Chanzo cha yote, na Mtegemezaji wa yote kupitia Mwanawe, Yesu Kristo. Mambo yote yamepangwa kuendana na mapenzi yake kwa ajili yake mwenyewe, ili aweze kupokea utukufu kwa mambo yote. • Kuonyesha namna kazi maalum ya uangalizi na utunzaji wa Mungu inavyofunuliwa katika utunzaji wake na usimamizi wa vitu vyote. • Kufafanua wazi ni makosa mangapi yanayohusiana na falsafa ya kisasa na dini yanatokana na kutoelewa kuhusu uangalizi na utunzaji wa Mungu juu ya uumbaji na historia. • Kuonyesha ufahamu wa vipengele muhimu vya utunzaji na utawala wa Mungu, pamoja na nia yake ya kurejesha uumbaji katika utukufu wake wa kwanza wakati wa kurudi kwa Kristo. • Kutoa maelezo mafupi ya jinsi gani uangalizi na utunzaji wa Mungu unavyotatua baadhi ya makosa ya kisasa ya falsafa na theolojia, hususan imani kwamba Mungu ni sawa na uumbaji wake ( pantheism ), imani kwamba Mungu aliyeumba ulimwengu hajihusishi tena na mambo ya ulimwengu ( deism ), mtazamo kwamba matukio yote ya zamani, ya sasa na ya baadaye, yamepangwa tayari na Mungu na kwa sababu hiyo hayawezi kuepukika ( fatalism ), na msimamo kwamba mambo yote hutokea kwa bahati nasibu ( chance ).

Malengo ya Somo

2

Made with FlippingBook - Online catalogs