Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook

4 6 /

M U N G U B A B A

Hakika ni Wa Aina yake

Ibada

1 Tim. 6:13-16 - Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato, 14 kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo, 15 ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana; 16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina. Neno sui generis (linatamkwa SUE-ee gin-air-us) ni msemo wa Kilatini unaomaanisha, “~a aina yake” au “~a tofauti katika kundi la vitu.” Ni kifupisho kinachomaanisha “~a pekee katika aina yake.” Hii ni njia nzuri ya kumwelezea Mungu mwema asiye na kikomo na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Mojawapo ya kweli muhimu sana kwa mwanamume au mwanamke wa Mungu ni dhana ya Mungu kama mwangalizi mkuu, anayefanya mambo yote kulingana na mapenzi yake mwenyewe. Ukweli huu, kwamba Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu ni Mungu mwenye kusudi kuu, ndio msingi hasa wa mafundisho mengine na maagizo mengine yote ya Maandiko. Kama Mungu wa kweli, aliyefanya na kuumba vitu vyote, Yehova anaweza kufanya apendavyo na yeyote amtakaye kwa sababu zozote zinazokubalika kwake. Haijalishi hali inaonekana ya kutisha kiasi gani, uhitaji ni mkubwa kiasi gani, mazingira yanaonekana ya kusikitisha kiasi gani, yeye ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Bwana wetu Yesu, Yeye yule ambaye huwafufua wafu na kubadili maisha yote kuelekea mapenzi na makusudi yake makuu. Ushahidi wa Biblia usioweza kupingwa ni kwamba Mungu wa Maandiko hakuumba ulimwengu na kisha akaenda zake mbali nao, ili ujipambanue kwa namna yoyote unavyotaka. Ingawa ameruhusu uovu kuwepo kwa kitambo, alianzisha mpango tangu mwanzo wa kuukomboa uumbaji wake kupitia Mwanawe Masihi Yesu. Sasa kwa kuwa Mwanawe amekamilisha ukombozi wake, amekusudia kwa wakati aliouchagua mwenyewe kipindi na majira ambayo mambo yote yatarudishwa chini ya utawala wake mkuu milele. Zaidi ya hayo, ameazimia kutimiza hayo yote kupitia Yeye aliyebarikiwa na Mwenye enzi kuu pekee, Mfalme Yesu, Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme. Kama vile Paulo anavyodokeza kwa Timotheo katika andiko letu hapo juu, ni Bwana wetu Yesu pekee akaaye katika nuru hiyo ya Baba yake, Mungu wa kweli, asiyepatikana na mauti, akaaye katika nuru isiyoweza kukaribiwa, nuru kuu ya roho safi ya kiungu, ambaye hakuna mwanadamu amewahi kumwona au awezaye kumwona. Mungu wetu ndiye Mungu wa kweli, Muumba mkuu wa ulimwengu mzima, anayefanya mambo yote kulingana na hekima na nguvu zake mwenyewe. Mapenzi yake yanaweza kupingwa lakini kamwe hayawezi kuzidiwa au kuzuiwa. Aliumba

2

Made with FlippingBook - Online catalogs