Mungu Baba, Swahili Module 6 Student Workbook
4 8 /
M U N G U B A B A
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za kukusanya
MIFANO YA REJEA
Hajui au Hajali
Wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana, katika kutoatoa maoni kuhusu kulipuka kwa bomu hatari la kigaidi hivi karibuni lililojeruhi watu wengi wasio na hatia, mmoja wa wafanyakazi wenzako anatafuta kukupenyeza katika mjadala. Huku akijua kuwa wewe ni Mkristo anasema, “Unawezaje kusema kwamba Mungu yupo wakati mambo haya mabaya yote yanawapata watu wasio na hatia kabisa? Haileti maana yoyote. Hebu tazama, kama Mungu anajua kuhusu mambo yote haya, anapaswa kuyazuia, si ndiyo? Kama anajua na hafanyi jambo lolote, basi sawa, anawezaje kuwajali watu hata kidogo? Umeona, haileti maana kabisa kwamba mambo haya yanaendelea kutokea pasipo Mungu kufanya jambo lolote kuhusu mambo haya!” Ikiwa macho yote yamekugeukia wewe na ukaambiwa uelezee kwa nini ipo hivyo, ungesemaje? Katika kuzungumza na mmoja wa vijana wenzako wa hapo mtaani, unashangaa kujua kwamba anaamini kwamba hakuna kusudi kuu la maisha, hakuna sababu hata moja au kusudi nyuma ya mambo yote. Anasema kwamba mambo pekee anayoyajua katika maisha haya ni huzuni na misiba; mambo hayajawahi kumwendea vizuri katika lolote, amekuwa wa mwisho mara zote, mara zote amekuwa bila furaha na hajawahi kuwa na furaha. Hawezi hata kufikiri kwamba nyakati zilizopita ni tofauti na hizi kwakuwa uzoefu wake unaakisiwa katika maisha ya wale wa nyumbani, na familia yake kubwa. Kwa yeye, anasema, msisimko wa maisha ni kama wimbo wa B.B King; Msisimko umetoweka. Je, tunawezaje kuzungumza na ndugu huyu kwa kujali hali yake pasipo kukubaliana na kuyakatia kwake tamaa maisha? Msisimko Umetoweka
1
2
2
Mungu ni Kila kitu na Kila Mahali
Katika moja ya vipindi vyake kwenye chuo cha vijana chipukizi, mmoja wa vijana wako katika darasa la Shule ya Jumapili hajui la kufanya kwa mwalimu wake ambaye anaamini kwamba Mungu ni sehemu ya ulimwengu mzima. Mwalimu alisema darasani, “Mungu yuko kila mahali na katika kila kitu. Hatuhitaji dini rasmi kwa sababu kila kitu ni kitakatifu, kwa maana kila kitu ni Mungu.” Je, mwanafunzi
3
Made with FlippingBook - Online catalogs