Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 1 0 1
M U N G U M W A N A
Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengine yaliyoibuliwa na video. Kwa njia nyingi, unyenyekevu na kujishusha kwa Bwana wetu ni kiini na kielelezo cha maadili yetu binafsi katika Ufalme wa Mungu. Tumeitwa kuteseka pamoja naye, kubeba msalaba wetu kila siku, na kumfuata. Ni pale tu tunapopata kushiriki katika mateso yake ndipo tunaweza kukombolewa kikamilifu kama vyombo vyake vya ibada na ushuhuda. Haiwezekani kutotilia maanani umuhimu wa msalaba na tukawa na uongozi wa kiroho au huduma bora katika maeneo ya mijini. Jibu maswali yafuatayo kwa dhumuni la kutumia kweli hizi namna Roho atakavyo kuongoza. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi na ujenge hoja zako kwa uthibitisho wa maandiko. 1. Nini maana ya kishazi “Yesu Kristo kujifanya kuwa hana utukufu?” Kwa maneno mengine, Yesu “alijiondoa” nini hasa katika Umwilisho na huduma yake duniani? 2. Maisha na huduma ya Yesu vilionyeshaje utumishi wake, unyenyekevu, na kujishusha kwake? Je, hili lina maaana gani katika maisha yetu wenyewe, ufuasi na huduma zetu leo? 3. Kuna uhusiano gani kati ya Yesu kujinyenyekeza na yeye kuacha “matumizi huru” ya sifa zake za kiungu alipokuwa duniani? 4. Kwa nini kifo cha Yesu ni muhimu sana kwa ufahamu wa jumla wa dhana ya Umwilisho? 5. Tunapaswa kuwa na uelewa gani kuhusu kifo cha Yesu kama dhabihu ya fidia kwa ajili ya ulimwengu? Elezea jibu lako. 6. Nini maana ya ukweli kwamba kifo cha Yesu ni upatanisho wa dhambi zetu? 7. Ni kwa njia gani kifo cha Yesu kwetu kina maana ya Pasaka na dhabihu mbadala? 8. Je, mzozo na mapambano kati ya kifo cha Yesu na shetani vinaonyesha sifa gani? Kwa maneno mengine, kifo cha Yesu kiliharibu kazi ya shetani kwa njia gani? 9. Kifo cha Yesu kimeletaje upatanisho kati ya Mungu na uumbaji wake na wanadamu, ukizingatia uumbaji na mwanadamu wameathiriwa sana na dhambi na laana?
Sehemu ya 1
Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
3
Made with FlippingBook - Online magazine maker